Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na kusudio lake la kuondoa kodi na tozo zinazokera wafanyakazi, hatoweza kupandisha mishahara ya watumishi kwa mwaka huu.
Rais Samia ameeleza hayo leo, jiini Mwanza katika maadhimisho ya Mei Mosi ambapo amesema binafsi anatamani kuona mishahara ya watumishi inaongezeka lakini kwa mwaka huu hatoweza kutimiza matamanio ya wafanyakazi, huku akieleza kuwa uchumi wa Tanzania umeshuka kutoka 6.9% hadi 4.7% kwasababu ya Corona.
''Ndugu zangu mimi ni mama, na mama ni mlezi, lakini kuna msemo wa kiswahili unasema 'masikini hampendi mwana', nataka nitamke wazi kuwa mimi binafsi natamani sana kuona mwaka huu mishahara ya watumishi ingeongezwa ila kwasababu mbalimbali nimeshinda kutimiza matamanio yenu,'' amesema Rais Samia
Awali Mhe. Samia ameeleza kuwa serikali imelifanyia kazi ombi la wafanyakazi kuhusu kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara kwa kupunguza asilimia moja ya makato ya Payee.
''Nataka niwaambie kwamba serikali imesikia ombi la wafanyakazi la kutaka kupunguza kodi inayokatwa kwenye mishahara, tumeamua kupunguza asilimia moja ya makato ya Payee kutoka asilimi 9, mimi na nyinyi wote sasa tutakatwa asilimia 8," amesema Rais Samia
from Author
Post a Comment