MWENYEKITI TPSF: WANAWAKE WA TWCC MSIJIFUNGIE NDANI |Shamteeblog.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

MWENYEKITI wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Angelina Ngalula amewaasa Wanawake wanaounda Chama cha Wafanyabiashara Wanawake nchini (TWCC) kuacha kujifungia ndani badala yake kutembea sehemu mbalimbali ili kukutana na watu waliofanikiwa katika ujasiriamali na biashara kiujumla.

Akizungumza na Wafanyabiashara wa TWCC jijini Dar es Salaam katika kikao chake cha kila mwenzi, Angelina amesema Wanawake hao wafanyabiashara, wajasiriamali wanapaswa kukutana ili kusaidiana mawazo katika biashara zao sambamba na kubadilishana mawazo katika biashara hizo.

“Tunapokutana tuwatafute Wanawake waliofanikiwa katika biashara, wapo wenye biashara zenye mitaji ya Shilingi Milioni 10, 20, 30, hao ndio tunatakiwa tuwatafute na tukae nao tubadilishane nao mawazo, tuwaulize wao walifanyaje hadi kufika hapo?”, amesema Angella 

“Wanawake tengenezeni bidhaa mbalimbali zenye kuleta ushindani ili kufikia malengo katika biashara zenu, ongezeni ubora wa bidhaa, lakini lazima ufanye biashara kwa kubadilisha bidhaa unazouza, sio mtu anauza bidhaa haitoki lakini ameng’ang’ania bidhaa hiyo hiyo”, ameeleza Angelina.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama hicho (TWCC),  Bi. Mercy Sila amesema kwa sasa Chama hicho kina ukaribu na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ikiwa ni pamoja na kufikisha changamoto za Wafanyabiashara Wanawake kupitia Taasisi hiyo.

Bi. Sila amesema kupitia Mwenyekiti huyo wa TPSF anaamini changamoto mbalimbali za Wafanyabiashara hao zikiwemo zile za Wafanyabiashara wa mipakani zitapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo kutokana na TPSF kufanya kazi kwa karibu na TWCC.

Kwa upande wake, Mwanachama wa TWCC, Bi. Hellen amesema mikutano kama hiyo kila mwezi inawapa fursa kama Wafanyabiashara kukutana pamoja na kujuana vizuri, kubadilishana mawazo katika biashara mbalimbali na kupata jukwaa pana katika kukuza na kuendeleza biashara wanazofanya.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Angelina Ngalula (aliyesimama) akizungumza na Wanachana wa TWCC katika mkutano wa kila mwezi uliowakutanisha Wanawake hao jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama hicho (TWCC),  Bi. Mercy Sila akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi kuzungumza na Wachama wa TWCC katika Mkutano wa kila mwezi uliofanyika Dar es Salaam
Baadhi ya Wanachama wa TWCC wakiendelea kusikiliza yanayoendelea katika mkutano wa kila mwezi uliofanyika Dar es Salaam.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post