NAIBU KATIBU MKUU DKT MDOE ASHANGAZWA NA BINTI ALIYEBUNI KIFAA KINACHOTOA TAARIFA SEHEMU IVUJAYO GESI KWENYE BOMBA |Shamteeblog.

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, anayeshughulikia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. James Mdoe akipata maelezo kutoka kwa  Naibu Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Dkt Prosper Mgaya kuhusu mfumo wa taa za  kuongozea Treni na magari uliobuniwa na mwanafunzi wa chuo hicho. Dkt Mdoe alitembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya  Ufundi leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Maonesho hayo yameandaliwa na  Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika Banda la Nacte kabla ya kuanza kutembelea maonesho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Nacte, Profesa Kondoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe (kulia) akitembelea banda la Chuo cha Taifa cha Utalii wakati wa maonesho hayo.
Dkt. Mdoe akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msaidizi wa Mipango ya Muda Mfupi wa Benki Kuu (BoT), Tulla Mwigune kuhusu alama mbalimbali muhimu zilizomo kwenye noti alipotembelea banda hilo.
Dkt. Mdoe akitembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza NACTE, Profesa Kondoro.
Meneja wa Kanda wa Kampuni ya Tera Technologies and Eng. Ltd. Christina Enrisha akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Mdoe  kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo ikiwemo mifumo ya ulinzi ya kielektroniki kama vile CCTV.

Dkt. Mdoe  akipata  maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Intermech Engineering Limited, Injinia Peter Chisawillo kuhusu mashine mbalimbali wanazozitengeneza za  kuchakata mazao ya kilimo.
Mkurugenzi Ukuzaji Mitaala na Upimaji wa NACTE, Dkt.Annastellah Sigwejo (kushoto) akiangalia kifaa maalumu cha kufugia samaki.


Dkt. Mdoe akiangalia mashine iliyobuniwa ya kupepeta mazao.
Dkt. Mdoe akizungumza kwa kutaka ufafanuzi alipotembelea Banda la Sugeco ambalo moja ya kazi zake kuwafanyia atamizi vijana kwa kuwatafutia masoko ya mazao wanayozalisha pamoja na kutengeneza vitalu nyumba vya kukausha mazao.Kushoto ni Mwatamizi wa  Sugeco, Fatuma Mbaga.


 Mwenyekiti wa Kikundi cha Kemmy Product, Penina Kaminyonge (kushoto) akimueleza Dkt. Mdoe kuhusu bidhaa zao mbalimbali wanavyosindika ambazo wanauza kwenye maonesho hayo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt James Mdoe ametembelea Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo amewapongeza wabunifu wa aina mbalimbali walioshiriki katika maonesho hayo ambapo ameshangazwa na msichana wa Chuo Kikuu cha St. Joseph ambaye amebuni kifaa kinachotoa taarifa sehemu ivujayo gesi  kwenye bomba.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Katibu Mkuu akizungumza baada ya kutembelea maonesho hayo, Mkurunzi wa Kampuni ya Intermech Engineering Limited, Injinia Peter Chisawillo akielezea ubunifu wa mashine mbalimbali za kusindika na kuchakata bidhaa za mazao mbalimbali lakini pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Ensol akielezea umuhimu wa wanafunzi wawapo shule kuzingatia masomo na mambo mengine kuhusu vifaa vya ulinzi vinavyotengenezwa na kampuni hiyo....


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post