NIC YADHAMINI DAR CITY MARATHON |Shamteeblog.

 


Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Isaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kudhamini Dar City Marathon zitazofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwaandaji wa Dar City Marathon Godfrey Mindu akitoa maelezo kuhusiana na marathon hiyo namna walivyojipanga katika suala la ulizi na taratibu za riadha zinavyofanyika.
Kaimu Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) Ombeni Zavara akizungumza kuhusiana na uratibu wa uandaji wa mbio unavyotakiwa kufuatwa, jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) pamoja na waandaji wa Dar City Marathon na uongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT).

*Zawadi  Nono za washindi zatangazwa

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limedhamini  mbio za Dar City Marathon zitazofanyika Mei 23 mwaka huu  katika Kiwanja Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Marathon hizo zinafanyika kwa nia ya kukuza vipaji pamoja na kujenga afya kwa wananchi na kuwa na nguvu kazi inayoweza kuzalisha katika kuendeleza uchumi wa nchi.

Hayo yamebainishwa Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Mteja wa NIC Isaya Mwakifulefule wakati akizungumza na  waandishi wa habari  kuhusiana na udhamini wa marathon hizo ikiwa pamoja na kutangaza shughuli zake za kuelewa faida za Bima pia kujenga afya za wananchi.

Amesema kuwa NIC wamekuwa sehemu ya jamii kusaidia  mambo mbalimbali yenye tija na  lengo la kukuza ajira kwa vijana nchini na kulinda afya zao.

Mwakifulefule amesema  pamoja na kutengeneza mawasiliano  ya wadau hivyo Dar City  Marathon wana malengo pamoja na Fedha hizo kwenda kwa wana marathon na kuwajengea uwezo katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

"NIC inashiriki kwa kutambua kuwa haiwezi kuiacha jamii ambayo ndio sehemu kubwa ya wadau na wanatumiaji wa  bima mbalimbali"amesema Mwakifulefule.

Mwakifulefule ametoa wito kwa watanzania kuendelea kujiandikisha kwa kujitokeza kwa wingi waje kushiriki mbio hizo kwani kushiriki kwao si tu watakimbia na kulinda afya zao huku washindi wakipata sehemu ya ajira yao.

Nae Mwandaji wa Dar City Marathon Godfrey Mindu  amewashukuru NIC kwa kuweza kuwa wadhamini katika mbio hizo hivyo wamekuwa na mchango mkubwa hasa katika kuleta furaha ya riadhaa kwa washiriki.

Hata hivyo amesema washiriki  Wanaume  na Wanawake kwa Mbio za Kilomita 21 wote watakaoshiriki watepewa tshirt za kukimbilia  pamoja na mshindi wa kwanza atapewa milioni moja, mshindi wa pili  Sh.750,000,Mshindi wa Tatu sh.500,000,Mshindi wa Nne Sh.300,000 Mshindi wa Tano Sh.200,000  pamoja na washindi wa Sita hadi 10 kila mmoja atapewa sh.100,000.

Washindi wa Kilomita 10  kwa Wanawake na Wanaume mshindi wa kwanza atapewa Sh.500,000 mshindi wa pili  Sh.375000,Mshindi wa Tatu sh.250,000,Mshindi wa Nne Sh.150,000, Mshindi wa Tano Sh.100,000  pamoja na washindi wa Sita hadi 10 kila mmoja atapewa sh.50,000.

Kwa upande wa Kilomita Tano watapewa Medali  pamoja na zawadi ya kuvaa Mkononi.

Kwa upande wa Kaimu Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT) Ombeni Zavara amesema kuwa mbio zote lazima zifuate taratibu na sio kuvuruga.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post