MREMBO mwenye figa matata Bongo, Nicole Joyberry hivi karibuni amefunguka kitu asichokipenda sana kwenye maisha yake kuwa ni umaarufu kwa sababu unamzuia kufanya mambo yake mengine ya kawaida.
Akizungumza na Risasi Vibes, mrembo huyo ambaye amewahi kutamba kwenye video ya wimbo wa Uno ya msanii wa Bongo Fleva Rajab Abdul ‘Harmonize’ ameendelea kusema kwamba anachukia umaarufu kwa sababu kuna wakati anatakiwa afanye vitu vikubwa ambavyo hana uwezo navyo, wakati yeye hajazoea hayo maisha.
“Mimi sipendi sana umaarufu kwa sababu una uongo mwingi, yaani ukiwa maarufu kuna muda unatakiwa uishi kama tajiri wakati wewe ni masikini jambo ambalo mimi silitaki kabisa, binafsi nimeshazoea kufanya mambo yangu ya kawaida, napenda kwenda sokoni mara kwa mara, nikiishiwa pesa nina uwezo hata wa kwenda kwa mangi nikakopa, lakini sasa ukiwa maarufu hivyo vitu vyote huwezi kuvifanya, utaogopa eti watu watakuona, sasa hayo maisha gani? Ndio maana mnaona huwa siposti mara kwa mara maisha yangu kazi wala biashara kwa sababu sijihesabii mimi kama ni maarufu sana kama walivyo wengine na napenda iendelee kuwa hivyo,” alisema Nicole.
from Author
Post a Comment