RAIS SAMIA AMEFANYA ZAIDI YA MATARAJIO KWA WAFANYAKAZI NCHINI |Shamteeblog.



Mei Mosi ni siku ya Wafanyakazi Duniani kote ambapo kitaifa imeongozwa na Rais wa sita awamu ya 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan zilizofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Matarajio ya wengi ni nyongeza ya mshahara lakini kwangu nimeona Rais Samia amefanya zaidi ya matarajio kwa Wafanyakazi na hata wasio Wafanyakazi.

Mosi; Rais Samia ameshusha kodi ya mshahara ama kodi ya lipa kwa kadri unavyopata "Pay As You Earn" (PAYEE) kwa asilimia moja (1%) toka 9% hadi kufika 8%. Hapa maana yake makato ya kodi ya mshahara yamepungua kwa 1% ambapo kiwango cha mshahara kitaongezeka tofauti na awali ilivyokuwa. Hii ni sehemu ya nyongeza ya mshahara.

Pili; Rais Samia amefuta retention fee ya 6% kwenye bodi ya mikopo waliyokuwa wakikatwa waliokopeshwa fedha za kusoma elimu ya juu. Maana yake kama ulikopa milioni moja itarudishwa milioni moja na sio milioni moja hiyo kuongezeka kwa 6% kwa mwaka kama haujamaliza deni lako. Hili ni goli la ushindi kwa Wafanyakazi wale wenye maumivu ya makato ya fedha za mikopo kwenye mishahara yao.

Tatu; Rais Samia amefungua promotion zote ambazo zilikuwa zimekwama tangu mwaka 2018. Leo hii kuna adjustment ya madaraja kwa wale wenye kustahili ambao walikosa kufanyiwa hivyo. Maana yake daraja likipanda na mshahara unapanda pia. Ni neema kwa Watumishi wa muda mrefu kwenye uongezekaji wa wanachopokea kwenye mishahara yao.

Nne; Rais Samia ameongeza umri wa utegemezi kutoka miaka 18 hadi miaka 21. Hii maana yake kuna nyongeza ya manufaa kwa wale wanao wategemea waajiriwa. Mathalani Mtoto tegemezi aliyekuwa akiishia kupata fursa ya matibabu ya bima ya afya hadi miaka 18 leo hii atakuwa na nyongeza ya miaka 3 ya manufaa ya matibabu ya afya. Hapa Rais Samia amemtua mzigo wa gharama za matibabu kwa Mfanyakazi kwa zaidi ya miaka 3 kwa yule ama wale wanaomtegemea. Ukitazama utegemezi unaotokana na extended families zetu utagundua Rais Samia amewaokoa sana Wafanyakazi.

Haya machache yananifanya nione Rais Samia amefanya zaidi ya matarajio. Aliyoyafanya Rais Samia ni zaidi ya kupandisha mishahara kwa siku zake chini ya 50% akiwa Ikulu. 


Na Emmanuel J. Shilatu




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post