UKOSEFU WA ELIMU YA UZALISHAJI WA MAZAO BORA NI CHANGAMOTO KUBWA KWA WADAU WA KILIMO |Shamteeblog.

 WADAU  wa mazao ya  kilimo cha Viungo, Mboga na Matunda Kiswani Pemba wamesema   ukosefu wa elimu ya uzalishaji wa mazao bora ndio changamoto  inayowafanya wazalishaji kushindwa  kuyafikia masoko hali inayo pelekea kushindwa kufikia malengo  walio kusudia.

Hayo yamebainishwa na wakulima katika kikao kazi cha kujadili changamoto zinazowakabili wakuluma na wafanyabiashara kisiwani Pemba ambapo wamesema kutokana na elimu duni walio nayo inapelekea kuzalisha mazao yasiyo kidhi viwango kulinganana maitaji ya soko.

Mbarouk Mohamed Hamad mmoja wa washiriki alisema wapo wakulima na wafanyabiashara wenye utayari wa kuzalisha kwa wingi lakini elimu ya usizalishaji wa mazao bora ni kikwazo zaidi ambacho kinapelekea kukata tama ya kuendelea na uzalishaji.

“Wakulima tuna bidhaa nyingi lakini tatizo lipo kwenye kuzifikisha bidhaa hizo sokoni zikiwa na ubora wake kwani kutokana na kukosa elimu ya uzalishaji bora wakulima wengi bado hawaoni kama kilimo ni sehemu ya kuongeza kipato,” alisema.

Nae Dadi Omar Dadi alibainisha changamoto nyingine kuwa ni uwepo wa tozo kubwa pamoja na gharama katika upatikanaji wa alama ya ubora wa bidhaa.

“Suala la tozo kwa wafanyabiashara na wakulima limekuwa ni tatizo hasa uwepo wa gharama kubwa ya kupata kibali cha alama ya ubora wa bidhaa kwani kama ambavyo tunafahamu huwezi kulifikia soko la kubwa kama huna nembo ya ZBS na wakulima na wafanya biashara wengi tunashindwa kufika huko kutokana na kukosa uthibitisho huo,”

Kwa upande wake Saleh Said Suleiman alisema usawa katika uhamasishaji wa taasisi zinazosimamia mazao ya kilimo kwa wakulima kuzalisha mazao yote ni mdogo kutokana na wataalamu kuegemea katika baadhi ya mazao machache.

Alisema, “serikali na taasisi nyingi zimeelekeza nguvu zaidi kuweka kipaumbele katika baadhi ya mazao hasa Karafuu na kuyaacha mazao mengine kukosa hamasa ya uzalishaji wake jambo ambalo linapekelea hata wale wakulima wanaojiingiza katika kilimo mfano cha mboga wanajikuta hawapati msaada wa kitalaam.”

Afisa kilimo Wilaya ya Chake Chake, Juma Khamis Rajab alisema licha ya kuwepo kwa uhaba wa wataalam wa kilimo lakini hata wale wachache waliopo wengi wao hawana taaluma ya ubobezi katika mazao mengi hasa viungo na matunda.

“Hata wale wataalamu wachache wa kilimo waliopo wengi wao hawana taaluma stahiki juu ya mazao hasa Viungo kutokana na mtaala wa elimu yao kujikita katika baadhi ya mazao tu. Unakuta bwanashamba elimu aliyotoka nayo chuoni miaka kumi iliyopita ni hiyo hiyo hawapati fursa ya kwenda kujiendeleza na matokeo yake wanageuka kuwa wanafunzi na kujifunza kutoka kwa wakulima badala yao kuwafundisha wakulima namna ya kulima,” alisema.

Kwa upande wake Dkt. Salim  Seleman Ali, kutoka Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) alisema wadau wanajukumu la kuungana pamoja kutoa maoni ya changamoto zinazowakabili katika sekta ya kilimo na biashara ili kuhakikisha lengo la kubadilisha sekta ya kilimo kuwa yenye tija kwa wakulima linafikiwa.

Alisema, “Ili lengo la mradi huu wa Voungo, Mboga na Matunda uweze kufanikiwa ni wajibu wetu wadau wa kilimo na biashara kuyazungumza matatizo yanayotukabili ili mwisho wa siku tujue namna ya kuzitatua.”

Mapema afisa anayeshughulika na kuwaunganisha  wadau katika mradi huo, Arafa Abdalla Juma alisema lengo la ujio wa mradi huo ni kuongezeka upatikanaji wa masoko ili kuwezesha kilimo chenye tija kwa wakulima.

“Mradi umejipanga kuhakikisha wakulima wanazalisha mazao ya kilimo kwa wingi na kuyafikisha katika soko sitahiki ambapo hilo litafikiwa kupitia uwekaji wa uwiano sawa wa bei ya mazao ya viungo, mboga na matunda.

Kikao hicho ni  mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Viungo, Mboga na Matunda  unao tekelezwa Zanzibar  na Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) People’s Development Forums (PDF), na Community Forests Pemba (CFP )  kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya (AU)  .


Mtaalam kutoka  Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Dkt. Salim  Seleman Ali akiendesha kikao
Baadhi ya washiriki wakiendelea na kikao.

  Dadi Omar Dadi msafirishaji wa mazao ya kilimo akichangia wakati wa kikao.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post