Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewatakia Heri na fanaka Waislamu Mkoa Kagera katika Kuelekea Sikukuu ya Eid El Fitr.
Katika salaam hizo ambazo zimeambata na Mkono wa Eid, zimewasilishwa kwa Niaba yake na Katibu wa Mkuu wa Mkoa Bwn. Sylvesta Raphael alipokwenda kukabidhi zawadi hizo kwa Makundi Maalum.
Akikabidhi zawadi hizo ambazo Ni Mchele, Mafuta pamoja Kitoweo Cha Mbuzi, Bwn Sylvesta amesema Mkuu huyo ambae yupo katika Majukumu mengine ya kikazi, anawatakieni Waislamu Heri ya Sikukuu na anawapongeza kwa kuhitimisha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani salama, na kuwaomba washerehekee kwa Amani.
Akipokea Mkono wa Eid Sheikh wa Mkoa Kagera Haruna Kichwabuta amefurahishwa na namna Mkuu wa Mkoa anavyozidi kuwakumbuka Waislam hasa Makundi Maalum, na kwamba zawadi hizo zimekuja muda muafaka hivyo zitawafikia walengwa.
Zawadi zilizotolewa ni pamoja na Kilogramu 200 za mchele, Mafuta ya kula Lita 100 na Mbuzi watano. Tayari zawadi hizo zimekabidhiwa kwa Sheikh wa Mkoa Kagera, Makao ya Watoto Yatima wa Nusuru Yatima Kashai, pamoja na Makao ya Wazee Kiilima.
By Mpekuzi
Post a Comment