RC SENDIGA AMEIGAIZA TRA IRINGA KUWASILISHA MAJINA YA WAFANYABISHARA WALIOSHINDWA KULIPA MADENI |Shamteeblog.



Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiongea na baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa chuo cha Afya kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamotoMkuu wa mkoa wa Iringa mh. Queen Sendiga akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiingia ukumbinu kuongea na baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara wa mkoa wa Iringa

Mfanyabiashara Dickson Lulandala akichangia maoni yake kwenye kikao cha pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alipokuwatana nao kwa mara ya kwanza.
Baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara na machinga mkoa wa Iringa waki msikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.





Mkuu wa mkoa wa Iringa mh. Queen Sendiga ameigaiza Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuwasilisha ofisini kwake majina ya wafanyabishara walioshindwa kulipa madeni yao baada ya makubaliano ya kisheria baina ya wafanyabiashara na mamlaka hiyo.

akizungumza kwenye kikao na wawakilisha wafanyabiashara na machinga wa mkoa wa Iringa alisema kuwa hata wafumbia macho wafanyabishara wote ambao tayari wamepewa maagizo ya kisheria kulipa madeni hayo lakini bado wamekuwa wanakaidi agizo hilo kutoka kwa mamlaka husika.

Akiwa katika kikao hicho mkuu wa mkoa wa Iringa alimuagiza meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuhakikisha anapeleka majina na kukutana na wafanyabiashara hao wanaokimbia kulipa madeni yao licha ya serikali kuagiza kulipa madeni hayo.

Mh: Sendiga alisema kuwa wadaiwa hao wakilipa kodi inachangia katika kuboresha sekta mbalimbali kama miundombinu, Afya, elimu, utalii, Ardhi, na kilimo katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi.

Alisema kuwa akaunti za wafanyabisha wakubwa ambao wanaodaiwa madeni makubwa zilikuwa zimefungwa hapo awali na kufunguliwa kwa mjibu wa sheria na makubaliano na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kulipa madeni hayo ili waendelee na biashara kama iliyokuwa awali.

Mh:Sendiga alisema kuwa jukumu la kulipa kodi ni kwa kila mwananchi anaishi nchini kwa lengo la kuchangia juhudi ya serikali kukuza uchumi wa wananchi na kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla hivyo wananchi wa mkoa wa Iringa wanatakiwa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka kuwa na madeni makubwa hapo baadae.

“Ngoja niwaambie kuwa bila kulipa kodi nchi haiwezi kukuza uchimi wake wala haitaweza kuleta maendeleo kwa wananchi kwa wakati kwa kuwa itakuwa inakosa fedha za kuanzisha miradi mikubwa ambayo inafaida kwa serikali” alisema Mh: Sendiga

Mh: Sendiga alimalizia kwa kuitaka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa kuhakikisha inatoa elimu ya mlipa kodi mara kwa mara ili kuepusha wafanyabiasha kufunga biashara zao au kushindwa kulipa madeni ya kodi wanayokuwa wanadaiwa.

Akipokea maagizo hayo meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Iringa Lamson Tulyanje alisema kuwa wameyapokea maagizo hayo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watayafanyia kazi ili kuwawezesha wafanyabishara hao kufanya biashara kwa uhuru na kukuza mitaji yao.

Tulyanje aliongeza kuwa watahakikisha wanaendelea kutoa elimu ya mlipa kodi mara kwa mara ili kuwakumbusha wafanyabishara kulipa kodi kuwa ni wajibu wao wa msingi kwa maendeleo ya nchini yao.

Tulyanje alisisitiza kuwa wananchi kudai risiti pale wanaponunua bidhaa yoyote kwa wafanyabishara hivyo hivyo kwa wafanyabiashara nao wanatakiwa kutoa risiti kwa wateja wao wanaonunua bidhaa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo mkoa wa Iringa Edmund Mkwawa aliwamuomba mkuu wa mkoa wa Iringa kuhakikisha anatatua changamoto za wafanyabiashara ili kukuza mitaji yao.

Alisema kuwa Iringa kunafursa nyingi za kibiashara ambazo zinaweza kukuza uchumi wa mkoa kwa haraka endapo changamoto walizozitoa zitafanyiwa kazi kwa kiwango kinachostahili.

Nao baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara mkoa wa Iringa wamtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga kuacha kusikiliza majungu ya baadhi ya wafanyabisha bali anatakiwa kujikita kutatua changamoto walizomueleza kwa lengo la kukuza uchumi wa mkoa huo.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post