Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC kimeanza kufanya maboresho ya
huduma za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa
taasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma za mfumo wa mahala
pamoja lengo likiwa ni kurahisisha utoaji wa vibali na leseni za
uwekezaji kwa kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la
uwekezaji nchini.
huduma za uwekezaji kwa kuunganisha mifumo ya kielektroniki kwa
taasisi na idara 11 za Serikali zinazotoa huduma za mfumo wa mahala
pamoja lengo likiwa ni kurahisisha utoaji wa vibali na leseni za
uwekezaji kwa kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la
uwekezaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Dkt.
Maduhu Kazi amesema maboresho hayo yatasaidia kuongeza ufanisi
katika kutoa huduma za wawekezaji na kuimarisha utendaji kazi wa
kituo hicho ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan alilolitoa Aprili, 2021 wakati akiwaapisha
makatibu wakuu wa Wizara.
Dkt Maduhu amefanya kikao cha pamoja na wakuu wa Taasisi na Idara
za Serikali 11 zinazotoa huduma kwenye Kituo cha huduma kwa
wawekezaji cha mahali pamoja (One Stop Facilitaion Centre) na
kubainisha kuwa mchakato wa maboresho hayo unaendelea kufanyiwa
kazi.
“Kama mnavyofahamu, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo ya namna ya
kuboresha huduma za uwekezaji, kikao hiki ni muendelezo wa
utekelezaji wa majukumu hayo, tulishaanza kuyafanyia kazi, na sasa
tunaendelea, lengo ni kutoa huduma bora zaidi za uwekezaji”
amesema Dkt. Maduhu.
Katika kikao hicho, Dkt. Maduhu amepokea taarifa ya hatua ambazo
zimechukuliwa kwa kila Taasisi na Idara husika zikiwepo kila taasisi
kufungua mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya utoaji vibali na leseni
mbalimbali, kuunganisha mifumo hiyo ili kuwa na dirisha moja la
huduma kwa wawekezaji nchini na taasisi husika kukamilisha hatua
zote ikiwepo kuchambua na kutoa maamuzi kwa maombi husika ya
wawekezaji.
Maboresho haya yanaelezwa kuwa yatawawezesha wawekezaji
wanaowekeza nchini kupata huduma kwa muda mfupi na kwa kutumia
gharama ndogo.
Baadhi ya Taasisi zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Uhamiaji,
Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TMDA), Mamlaka ya Mapato Tanzani (TRA), Baraza la
Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) naOfisi ya Waziri Mkuu
(Kazi).
By Mpekuzi
Post a Comment