WABUNGE AEISH, KIRUMBA NA DITOPILE WAFUTURISHA WANANCHI WA JIMBO LA MAKAMU WA RAIS |Shamteeblog.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile akipika futari iliyoandaliwa na wabunge waliopo kwenye Timu ya Kampeni ya CCM Jimbo la Buhigwe.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Santiel Kirumba akiwahudumia wananchi wa Wilaya ya Buhigwe katika futari iliyoandaliwa na wabunge wa CCM waliopo kwenye timu ya kampeni Jimbo la Buhigwe.
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeish Hillaly akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kufuturu pamoja katika futari iliyoandaliwa na wabunge wa CCM waliopo kwenye kampeni za Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.
 

 Charles James, Michuzi TV

WABUNGE wa Chama cha Mapinduzi waliopo kwenye kampeni za ubunge Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma wamewaomba wananchi wa jimbo hilo kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake wanapotekeleza majukumu yao ya kuiletea Tanzania maendeleo.

Wito huo wameutoa wakati waliposhiriki futari ya pamoja na wananchi hao waliyoiandaa ikiwa imebaki siku moja kuelekea kilele cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika Futari hiyo wabunge hao walioongozwa na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeish Hillaly, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Sentiel Kirumba ambapo waliwaomba wananchi hao kutosi

kiliza maneno ya uchonganishi yanayotolewa na baadhi ya wanasiasa wenye lengo la kuharibu umoja na mshikamano uliopo kwa watanzania.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeish Hillaly amesema futari hiyo wameiandaa kama sehemu ya kuonesha kuwa watanzania wote ni ndugu licha ya tofauti za kiimani na kiitikadi zilizokuepo.

“ Tunawashukuru sana kwa kukubali kushiriki nasi katika futari hii tuliyoiandaa, mmeonesha moyo wa upendo ambao ndio sifa kuu ya watanzania, niwasihi msisikilize maneno ya uchonganishi yanayotolewa na wanasiasa waliokosa sifa hii ya upendo.

Mnafahamu Mei 16 ni Uchaguzi w kampeni hapa kwenu, na hili ni jimbo la Makamu wa Rais, niwaombe mkapige kura kwa wingi kama sehemu ya haki yenu kikatiba na mumchague Mbunge ambaye ataenda kuwaunganisha vema na Rais Samia na Makamu wa Rais Dk Mpango,” Amesema Aeish.

Jimbo la Buhigwe limeingia kwenye kampeni baada ya aliyekua Mbunge wake, Dk Philip Mpango kuteuliwa kushika nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post