SALAMU ZA SHUKRANI KUTOKA KWA FAMILIA YA MAREHEMU ISMAIL ISSA MICHUZI |Shamteeblog.



 FAMILIA ya Marehemu Mzee Maneno Issa inatoa shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na jirani kwa kuwa pamoja nasi katika msiba wa mpendwa wetu Ismail Issa Michuzi aliyefariki dunia siku ya Alhamisi tarehe 03/06/2021  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa siku ya Ijumaa tarehe 04/06/2021 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

Kipekee familia inatoa shukurani kwa madaktari na wauguzi katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe, Makandana mjini Tukuyu, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hususan kitengo cha dharura chini ya Dkt Juma Mfinanga na Dkt Suphiani, kwa kujitoa kwa moyo wote kujaribu kuokoa maisha ya mpendwa wetu. 

Salaam hizi pia ziwafikie uongozi wa Chai FM kwa kujitoa ka hali na mali wakati wa kuugua na hatimaye kifo cha ndugu yetu. 

Ni vigumu kumtaja na kumshukuru kila mmoja wenu kwani ni wengi mno. Hivyo itoshe tu kusema familia hii inawashukuruni sana sana kwa moyo wa upendo mliounesha kwetu. Hatuna cha kuwalipa ila ni Mola pekee atayewalipa.

ASANTENI SANA NA MBARIKIWE.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post