Charles James, Michuzi TV
ALIYEKUWA Mjumbe wa Bodi ya Usajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Milton Erasto amempongeza Waziri wa Afya, Dk Dorothy Gwajima kwa kuunda Kamati ya wajumbe ili kuhakikisha wanasimamia uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Amesema agizo hilo limekuja kutokana na uongozi uliopo kushindwa kutekeleza maagizo waliyopewa mara tatu mafululizo.
Milton ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizugumza na wandishi wa habari ambapo ameeleza kufurahishwa na agizo hilo la Waziri Dk Gwajima akisema limezingatia sheria.
“ Nimesikia Waziri Gwajima ameunda kamati ya ufuatiliaji na kamati ya uchaguzi ni jambo zuri sana kwa sababu huko nyuma uchaguzi haukufanyika na Waziri asirudi nyuma kwasababu sekta hii ikihimarishwa vizuri itakuwa na mchango mkubwa kwa Taifa,” Amesema Milton.
Ameongeza kuwa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mara ya mwisho lilifanya Uchaguzi wake mwaka 2016, ambapo kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi, viongozi hao muda wao wa kukaa madarakani uliisha mwaka 2019.
Milton ambaye pia ni Rais wa Muungano wa Wapiga kura Tanzania amesema sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali imekuwa na mchango mkubwa kwa taifa hili kwa sababu imekuwa ikiisaidia serikali katika masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na kidini.
Amesema pia amefurahishwa baada ya kusikia katika uchaguzi Wanawake nafasi ya ujumbe wa baraza Wanawake wengi wameshinda na kusisitiza waendelee kuungwa mkono.
“Imenitia moyo kwasababu akina Baba wengi wamebwagwa kwa sababu Wanawake wengi wameendelea kuvutiwa na uongozi wa kinara wao ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na uongozi wake mzuri ndani ya kipindi kichache alichokaa madarakani,”Amesema Milton.
Aliyekua Mjumbe wa Bodi ya Usajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), Erasto Milton akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali.
By Mpekuzi
Post a Comment