* Kifaa hicho kinatumia mwanga wa jua na kutoa sauti.
Na Chalila Kibuda
CHUO cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Mikumi kimegundua kifaa cha kufukuza ndege shambani 'Sound Birds Scare, lengo ikiwa kuwarahishia wakulima kupiga kelele na gharama kwa ajili rasilimali watu panapokuwa na ongezeko la ndege wengi waonaharibu mazao ya nafaka.
Akizungumzia jijini Dar es Salaam leo katika Maonyesho ya ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambayo yameanza jana Mbunifu kutoka VETA Jonas Hokororo amesema kifaa hicho kitaondoa changamoto ya ya watu Kulinda huku baadhi wazazi kutuma wanafunzi kwenda kufukuza ndege shambani badala kwenda shule.
Mbunifu huyo ambaye pia ni Mwalimu wa chuo cha VETA Mikumi mkoani Morogoro amesema kuwa kipindi cha ndege wazazi wengi wanawaambie watoto wasiende shule ili wakafukuze ndege hao shambaini wanaoshambulia mazao.
Anesema kama VETA waliangalia ni njia gani ya kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo yao bila kukosa badala ya kwenda shambani kufukuza ndege.
Hokororo amesema kuwa alichoweza kubuni ni pamoja na sauti ambazo ndege wadogo wanaogopa ambao ni Mwewe,Kipanga.
Amesema kuwa kuna wakati alilima shamba la mpunga na kuona changamoto ya ulinzi wa ndege na kuamua kubuni kifaa hicho ambacho gharama yake ni shilingi 150,000.
Hokororo amebainisha kuwa kwa kawaida kuna ndege ambaye anakula ndege wadogo hivyo wakatengeneza kifaa hicho chenye sauti ya ndege jamii ya nwewe ambaye anaogopwa na ndege hao wadogo.
"Kutokana na changamoto ya utoro shuleni nikamua kugundua kifaa hiki ili kuwafanya wanafunzi waendelee na masoma yao badala ya kwenda shamba kufukuza ndege kwani kifaa hiki kinalidwa na mtu mmoja baba na mama akaendelea kupika vitumbua huku wanafunzi nao wakiendelea na masomo yao." Amesema.
Hokororo ameongeza kuwa kifaa hicho kinatumika kulinda aina zote za mazao ya nafaka na kwamba kuanzia mkulima anapo panda mbegu zake mpaka mavuno.
Aidha amewataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo ya kifaa hicho ambacho kinapunguza kundi kubwa la watu kwenda na badala yake kuendelea na majukumu mengine ya kujiongezea kipato kwa wanafamilia.
By Mpekuzi
Post a Comment