Hakainde Hichilema ashinda uchaguzi wa rais Zambia |Shamteeblog.
Mwanasiasa mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, 59, ameibuka mshindi wa uchaguzi uliofanyika Agosti 12 dhidi ya rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu, tume ya uchaguzi imetangaza.
"Ninamtangaza Hakainde Hichilema rais mteule wa Jamhuri ya Zambia ." Esau Chulu, mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, ametangaza .
Amemshinda mpinzani wake, rais aliye madarakani Edgar Lungu, kwa kupata kura milioni 2.8, sawa na kura milioni moja ikilinganishwa na alizopata rais aliye madarakani.
Ni eneo moja tu kati ya maeneo 156 katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambayo kura zake hazijahesabiwa rasmi, lakini tume hiyo imebaini kwamba hata kama kura hizo hazijahesabiwa, hilo haliwezi "kuvuruga ushindi wa Hichilema.
By Author
Post a Comment