Rais wa Afghanistan aikimbia nchi baada ya Taliban kuuteka mji mkuu |Shamteeblog.


Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameikimbia nchi yake jana jioni baada ya wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa Kabul. 

Maafisa wawili wa serikali ambao hawakutaka majina yao kutajwa wameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Ghani ameondoka Afghanistan na inaarifiwa amekimbilia taifa jirani la Tajikistan. 

Kuondoka kwa Ghani kunatoa taswira halisi ya uwezekano wa kundi la Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan .

.Wapiganaji wa kundi hilo waliingia kwenye viunga vya pembezoni mwa mji mkuu wa Kabul jana Alfajiri baada ya kupata mafanikio makubwa katika siku za karibuni kwa kuikamata miji mingi nchini humo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post