Injinia Yusuf Ismail Meneja wa Tanesco wilaya ya Ilala akizungumza na wananchi wa mtaa wa Vuleni Chanika Kata ya Msongola wilayani Ilala wakati Maofisa wa Shirika la Tanesco walipokuwa wakitoa elimu kuhusu uelewa wa shughuli za Tanesco na namna itakavyotekeleza mradi wa usambazaji wa umeme katika mtaa wa Mvuleni Chanika wilayani Ilala. jana Agosti 16, 2021 kulia ni Injini Nickson Babu Meneja wa wilaya ya Kitanesco ya Chanika
Injinia Yusuf Ismail amesema wao kama watendaji wa Tanesco ni watumishi wa wananchi hivyo niwawajibu wa wananchi hao kuwatuma ili waweze kuwatumikia kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo wa kuwasambazia umeme katika maeneo yao.
Injinia Yusuf Ismail ameyasema hayo wakati wa kikao cha kuwajengea uelewa wananchi wa Mvuleni Chanika wilaya ya Ilala jana kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika mtaa huo.
"Tumekuja kwenu leo ili kuwasikiliza kikao hiki sisi hatutakuwa wazungumzaji, tunawaachia nyie mzungumza na kutuambia changamoto na mambo mbalimbali mnayoona yanwezakuwa kikwazo wakati tutakapokuwa tukitekeleza jukumu la usambazaji wa ememe katika maeneo yenu,". Amesema Injini Yusuf Ismail.
Ameongeza kuwa hii ziara imetokana na mmoja wenu kuwa jasiri wa kupita katika ofisi mbalimbali kwa hiyo mseme nyie kama kuna kero na changamoto ili tuweze kuzitatua kwa sababu tunataka tusikilize kama kuna shida tutatue.
Ameongeza kuwa katika kilomita 10 ambazo zinatakiwa kusambazwa kwa kuanzia Tanesco itatekeleza mradi huo kwa kusambaza Kilomita 3.6 za miundombinu na baada ya hapo kila mtu ambaye yuko karibu na nguzo maana yake ataunganishwa na kupata umeme.
Ameonya wananchi wanaotumia mafundi vishoka kuacha mara moja tabia hiyo badala yake watumie taratibu zilizowekwa na shirika la umeme Tanesco ili kusambaziwa umeme, Na si vinginevyo kwani kuwatumia vishoka ni kuvunja sheria na unaweza kuingia kwenye mikono wa sheria.
Naye Afisa Usalama wa Tanesco Wilaya ya Ilala Bw. Steven Maganga akizungumza katika kutano huo aliwapatia wananchi wa Mvuleni namba zake za simu na kuwaagiza kutoa taarifa kwake mara moja au ofisi za Tanesco wilaya ya Ilala mara wanapoona kuna mazingira ya rushwa au hujuma zozote wakati wa utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha mradi unatekelezwa bila vikwazo na wananchi wanapata umeme kama ilivyokusudiwa na serikali.
Injini Nickson Babu Meneja wa wilaya ya Kitanesco ya Chanika akifafanua mambo mbalimbali namna watakavyotekeleza mradi wa usambazaji wa umeme katika mtaa wa Mvuleni Chanika na namna wananchi wanavyoweza kuepuka na kwasilisha kwao changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi huo kulia ni Steven Maganga Afisa Usalama Tanesco wilaya ya Ilala na kushoto ni Injinia Yusuf Ismail Meneja wa Tanesco wilaya ya Ilala.
Steven Maganga Afisa Usalama Tanesco wilaya ya Ilala akiwaelezea wananchi wa Mvuleni kuhakikisha wanachukua hatua kwa kutoa taarifa endapo wataona mazingira ya rushwa wakati wa utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme katika mtaa wao.
Hidaya Juma Afisa Mtendaji Mtaa wa Mvuleni Chanika akielezea jambo katika mkutano huo.
Bw. Khamis Kombo Mwenyekiti wa Mtaa wa Mvuleni Chanika ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho akiwafafanulia jambo wananchi waliojitokeza ili kupata elimu hiyo kutoka Shirka la Umeme Tanzania Tanesco.
Tumaini Mahwaya Afisa Huduma kwa wateja Msaidizi Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Ilala akiwaelezea wananchi wa mvuleni namna huduma za Tanesco zinavyotolewa kwa ubora ili kuwahudumia wananchi.
Elly Makala Afisa Uchunguzi Mwandamizi TAKUKURU Ilala akiwaelezea wananchi namna wanavyoweza kutoa taarifa kwa taasisi hiyo endapo kutaonekana mazingira ya rushwa katika utekelezaji wa mradi huo wa kusambaza umeme katika mtaa wa Mvuleni Chanika wilayani Ilala.
Wananchi mbalimbali wakiwa katika kikao hicho kilichoandaiwa na Shirika la Umeme Tanzania Tanesco katika kuwaandaa wananchi kupokea utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme katika mtaa wa Mvuleni Chanika wilayani Ilala.
Mmoja wa wananchi wa maa wa Mvuleni akitoa maoni yake wakati wa kikao hicho kilichofanyika mtaani hapo jana.
By Mpekuzi
Post a Comment