MWANAMAMA Zarinah Hassan au Zari The Boss Lady ambaye ni baby mama wa staa wa muziki Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amegeuka adui kwa kile alichokifanya ambacho hakikutarajiwa kama siku moja anaweza kuja kukifanya.
Zari ambaye amezaa watoto wawili na Diamond au Mondi; kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaondoa (un-follow) familia ya jamaa huyo kuwa miongoni mwa wafuasi wake ambao awali walikuwa wafuasi wake.
Zari amewaondoa watu wote ambao anadaiwa kusema anawaona hawana faida kwenye maisha yake na kubaki na watu tisa pekee wakiwemo watoto wake, Tiffah Dangote na Prince Nillan.
Zari amewapiga teke watu wote wa familia ya Mondi akiwemo Diamond mwenyewe na mama yake, Mama Dangote, Esma Platnumz na Rommy Jons ambao ni dada na kaka wa jamaa huyo na wengine wote wanahusiana na familia hiyo kama Juma Lokole, Ricardo Momo, Babu Tale na wengine wote.
Kwa mujibu wa Zari, ameamua kujipa nafasi zaidi na siyo kuwa karibu na watu ambao hawamsaidii chochote hivyo anataka kufanya mambo yake kivyakevyake.
Zari anasema, pamoja na kufanya hivyo, lakini anabaki kuwa mwanamke yuleyule na jina lilelile, lakini anakuwa na mawazo tofauti na mchezo mpya kabisa kwenye maisha yake.
Habari kutoka upande wa pili; yaani familia ya Mondi zinadai kuwa jambo hilo limewachukiza ambapo Esma amemjibu; “Ili ufanikiwe unahitaji marafiki, lakini ili ufanikiwe zaidi unahitaji maadui… ni rahisi tu!”
STORI: MEMORISE RICHARD, DAR
from Author
Post a Comment