*Doriye asisitiza kwenda kutoa huduma za bima kwa viwango vya kimataifa.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye amesema kuwa Shirika limekuwa imara kwa miaka mitatu iliyopita hivyo mwaka 2021 unaisha ni kazi kwa watumishi kuachana na mafanikio hayo na kujenga msingi mwingine wa mafanikio makubwa sana kwa mwaka 2022.
"Sisi ndiyo Bima hivyo katika soko hakuna wa kushindana nao ndio maana tumebadili mtazamo wa kufanya mteja kuwa kipaumbele kwa kuangaliwa kiti chake hata kama hayupo katika kiti hicho" amesema Doriye
Amesema watumishi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC ) wametakiwa kujiandaa kwenda na mabadiliko yatayojitokeza katika soko kwa mwaka mpya wa 2022 ili kuweza kuinua na kuendelea kuwa juu katika kutoa huduma kwa watanzania wenye shirika lao.
Dk.Doriye aliyasema hayo wakati alipokutana na Watumishi wa NIC kuajili ya kufunga mwaka 2021 na kwenda na mwaka 2022 kwa kuingia kwenye soko kwa kishindo kutokana bidhaa zilizopo kwenye shirika hilo.
Amesema mwaka mpya wa 2022 watumishi wa NIC watangulize ubunifu na uadilifu wa hali ya juu kwa kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa.
" Kuanzia mwaka 2002 NIC imekuwa ikikuwa katika utoaji huduma zake mpaka hivi leo lakini mwaka ujao unapaswa kuwa bora zaidi kushinda miaka yote iliyopita kwa kuongeza ufanisi katika kazi ikiwa ni pamoja na juhudi binafsi za kila mmoja na timu kazi" Amesema Dk.Doriye.
Amesema kumaliza mwaka ni kumshukuru Mungu kwa kuwa pamoja wakiwa salama na wamoja katika utendaji kazi ambao umekuwa chachu katika ujenzi wa taifa.
Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema katika ushindani wa soko ni kuongeza mikakati ya kuwafikia wateja kila kona ya nchi na wanaosajiliwa waone walikuwa wapi kusajiliwa na NIC.
By Mpekuzi
Post a Comment