Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya 'Shangwe Lipo Pale pale' yatoa zawadi za ada kwa washindi kumi imetoa |Shamteeblog.

Kampuni ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya "Shangwe Lipo Pale pale" imetoa zawadi za Ada kwa washindi kumi wa promosheni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mbagala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mmoja kati ya washindi aliyejishindia ADA ya shule kwa watoto wake, Jackline Macha mkazi wa Kibamba alisema "kwa kweli sikuweza kuamini mara nilipopigiwa simu kutoka Vodacom nikiwa kwenye shughuli zangu za kila siku na kuambiwa umejishindia zawadi kutoka Vodacom, nilifurahi sana kwa kuwezeshwa, maana ilinipunguzia mzigo huu wa ADA kwa mwaka huu, ambao kwangu ulikuwa mkubwa sana" . Nawashukuru sana Vodacom kwa zawadi hii na naomba nitoe wito kwa watanzania watumie mtandao wa vodacom kupitia huduma yake ya Mpesa kila mara.

Nae Meneja wa Mauzo Mwandamizi wa Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, George Nyanda alisema " Hii ni fursa kwa watanzania kujishindia zawadi mbalimbali kupitia promosheni yetu ya Shangwe Lipo pale pale, ambayo tumeianza mwezi Novemba mwaka jana kama "Show Love Tule Shangwe" kwa kuwapa wateja wetu zawadi, ikiwa ni wewe na umpendae kwa msimu wa sikukuu ya Christmass na mwaka mpya na sasa tumeenda mbali zaidi kwa miezi hii ya mwanzoni mwa mwaka tumeamua kutoa ADA ili ziweze kuwasaidia wazazi na walezi kupata nafuu ya watoto wao, ambao wataweza kuwalipia ADA na hivyo waweze kwenda shule bila tatizo". aliongeza Nyanda.

Jumla ya washindi kumi wa Ada, washindi kumi wa simu na washindi wanne wa Tv walipatikana, ili uweze kujishindia zawadi unatakiwa kutumia huduma ya M-Pesa kwa kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo kwa M-pesa kwa kupitia namba *149*01#





Meneja wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam, George Nyanda akizungumza na wakazi wa Mbagala wakati wa makabidhiano ya zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni ya Shangwe Lipo palepale iliyofanyika viwanja vya stendi ya mabasi Mbagala





By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post