Adeladius Makwega,DODOMA.
Wanakwaya Wakatoliki wametakiwa kuimba kwa uadilifu kama maelekezo ya liturujia ya kanisa hilo inavyoelekeza na siyo kuimba tu kimwili. Kauli hiyo imetolewa na Padri John Mapalala, Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikiria Maria Imakulata ya Chamwino Ikulu, Jimbo Katoliki la Dodoma Februari 6, 2022 katika misa ya pili ya dominika hiyo.
“Nimesikia wanakwaya wamesifiwa kwa kuimba vizuri, kuimba vizuri lazima kuendane na mafundisho ya kanisa letu maana sasa wengi wanaimba lakini lazima kuimba kwetu kuwa kama alivyofundisha Yesu Kristo.”
Je kwaya zetu sasa zinavyoimba ni sawa na muziki wa Kristo? Aliuliza huku wanakawaya hao waliomba jumapili hii wakitabasamu na kuguna.
“Muziki maana yake uwazi, lazima tunavyoimba maneno yetu yote yasikike na yaeleweke kwa wote, liturujia inatufundisha kuwa muziki wa injili maana yake ni uwazi wa Mungu, maneno haya yanayoimbwa yasikike kweli na siyo kwa kundi la wanakwaya tu, mmenielewa vijana? Maana huo ni muziki mtakatifu.”
Katika misa hiyo kwaya ya Shule ya Sekondari ya Chamwino ambayo ni kwaya ya wanafunzi wa shule ya serikali ya Kutwa na Bweni Wilayani Chamwino iliyo jirani na kanisa hil.
Awali kabla misa haijaisha, msomaji wa matangazo alisema kuwa Kwaya ya Shule ya Sekondari ya Chamwino iliimba vizuri na huku waamini wakiipigia makofi mengi ya pongezi na vigelegele. Kwa desturi ya misa vigelegele hivyo hupigwa katika nyimbo za shangwe(kushangilia) au pale inapotolewa pongezi kama ilivyotolewa na msomaji wa matangazo ya jumapili hii
“Waamini tunawaombeni jumapili ijayo kujiandaa na kumuaga katekista wetu wa Kigango cha Msanga ambaye amestaafu, hivyo tunawaomba kila mmoja aje na chochote cha kumuaga katekista wetu.”
Kandoni mwa misa hiyo hali ya hewa ya Chamwino Ikulu na maeneo jirani kwa juma zima ilikuwa na mvua za hapa na pale huku jua likiwaka kwa kadili na kuwasaidia mno wakulima waliopanda mahindi, kunde, matikiti, maboga na mazao mengine kukua kwa haraka.
Mwandishi wa habari hii alishuhudia njiani mazao haya yakibadili mandhari ya ukavu kuwa na madhari ya chanikiwiti ambayo ni nadra sana kuiona katika mkoa wa Dodoma.
Huku mahindi yaliyoota yakiwa na wastani wa urefu kati ya inchi 3-6, na kama hali ya hii ikiendelea hivyo basi wakulima wengi wataanza kuvuna mbogamboga kama mlenda, majani ya kunde na maboga baada ya juma moja kuanzia sasa katika maeneo mengi ya Chamwino Ikulu.
Hii ni ishara tosha kuwa pengine chakula cha kutosha kitapatikana kwa mavuno ya mwaka huu.
By Mpekuzi
Post a Comment