Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
-"Katika hali ya uandikishaji inayoendelea,Kibaha Mjini mpaka kufikia imeandikisha jumla ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 3,987 sawa na Asilimia 88.3 ya maoteo ya Wanafunzi 4,514.
Aidha,wavulana walioandikishwa ni 2011 ambayo ni asilimia 88.7 ya malengo ya kuwaandikisha 2,266 huku wasichana wakiwa ni 1,976 sawa na Asilimia 87.9 ya malengo ya kuwaandikisha 2,248.
Bado uandikishaji unaendeleaje kwa mujibu wa taratibu zilizopo"Eng.Mshamu Munde Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kibaha
"Kwa upande wa Elimu ya Msingi,Kibaha Mji inatarajia kuandikisha Wanafunzi 5763.Mpaka Februari 10,2022 Wanafunzi 5519 sawa na Asilimia 95.77 wameandikishwa.
Katika idadi hiyo wavulana ni 2826 sawa na 101.4 asilimia na wasichana ni 2693 ambayo ni 95.77 asilimia ya malengo ya wanafunzi 2977.Uandikishaji unaendelea....Eng.Mshamu Munde Mkurugenzi Kibaha Mji.
"Kwa upande wa Elimu ya Awali,Kibaha Mji mpaka Sasa imeandikisha jumla ya Wanafunzi 2,530 sawa na Asilimia 68.6 kati ya maoteo ya watoto 3,687.Kati yake wavulana ni 1,306 ambayo ni asilimia 71.8 ya watoto 1,822 wanaotarajiwa na Wasichana ni 1224 sawa na asilimia 65.63 ya matarajio ya Watoto 1865.
Aidha,uandikishaji huu umehusisha wenye mahitaji maalum na unaendelea mpaka Mwezi Machi,2022" Eng.Mshamu Munde,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha.
By Mpekuzi
Post a Comment