Raia wa Urusi waandamana kupinga uvamizi wa Ukraine |Shamteeblog.

Katika kile kinachoonekana kupinga uvamizi wa kivita wa nchi yao huko Ukraine, zaidi ya watu 1700 wamekamatwa kutokana na kufanya maandamano nchini Urusi.

Wananchi hao wameingia mtaani na kukutana na dola.

Wananchi wengi wameshangaa kwa nchi yao kuanzisha vita hiyo kubwa kwa majirani zao Ukraine ambao wamewaita kama ‘ndugu zao’.

Huko mjini Moscow, polisi pia wametanda kuzuia watu kukutana katika eneo maalum lililotengwa.

Na polisi wametumia vipaza sauti kuwataka watu kutawanyika.

Na katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo , St.Petersburg, polisi pia imewatawanya waandamanaji.

The post Raia wa Urusi waandamana kupinga uvamizi wa Ukraine appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post