KIKOSI cha Simba tayari kimeingia mjini Berkane, kikitokea Casablanca tayari kwa mechi yao dhidi ya wenyeji RS Berkane.
Mechi hiyo ni ya mchezo wa kombe la Shirikisho la Afrika.
Simba imesema imetua salama Berkane , huku wachezaji wakiwa sawa kimwili na kiakili kwa ajili ya mechi yao hiyo muhimu ya ugenini
Tayari Simba ina mtaji wa pointi 4 katika kundi lake baada ya kushinda mchezo dhidi ya ASEC Mimosas kwa mabao 3-1 huku wakitoka sare ya bao 1-1 na US Gendarmerie.
Habari kutoka katika kambi ya Simba zinasema kila kitu kipo sawa kwa mchezo huo hapo kesho.
Na leo Simba wanategemewa kufanya mazoezi katika uwanja ambao watacheza mchezo huo ili kuuzoea.
Taarifa zinasema huenda Jonas Mkude akaendelea kukosekana kutokana na afya yake kutotengamaa vizuri kwa sasa.
Mwingine ni Clatous Chama, ambaye usajili wake wa dirisha dogo unahusu michezo ya ndani tu.
Lakini uwepo wake katika kikosi kwa namna moja au nyingine unaweza kuisaidia Simba sababu anaijua vizuri RS Berkane, timu ambayo alikuwa akiichezea kabla ya kurejea Simba.
The post Simba ‘ ndani’ ya Berkane appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment