Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake wanaoishi Ukraine |Shamteeblog.

Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Urusi, Kyiv umewataka raia wake kuondoka nchini humo kwa sababu ya vita inayoendelea.

Katika taarifa yake ya jana usiku, ubalozi huo pia umewataka raia wake wale watakaoshindwa kufanya hivyo basi kufuatilia matangazo yanayotolewa na serikali mara kwa mara.

“Mfuatilie matangazo pale yanapotolewa juu ya tahadhari ya kutokea shambulizi,” umesema ubalozi huo.

Hali inazidi kuwa tete katika vita hiyo na Marekani imesema vikosi vya Urusi vinakaribia kuuteka mji huo mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Na tayari mamlaza za Ukraine zimezuia ndege zote za kimataifa kuingia sababu ya vita.

The post Marekani yatoa tahadhari kwa raia wake wanaoishi Ukraine appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post