Ukraine: Hakuna msaada kutoka kwa washirika wetu |Shamteeblog.

Katika hali ya kuonekana kukosa msaada, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametoa ujumbe kwa njia ya video akiwalaumu washirika wake kwa kuiachia nchi yake ipambane yenyewe.

Ukraine inaonekana kuhitaji msaada wa kupambana na taifa la Urusi lenye nguvu.

Hivi karibuni, Rais huyo aliwaomba wanaume nchini humo kutoondoka na badala yake wabaki kuipigania nchi yao.

” Asubuhi ya leo tena tunapambana wenyewe, kama ilivyokuwa jana,”.

“Taifa lenye nguvu zaidi duniani limekaa mbali likiangalia,” amesema Rais hiyo kupitia Facebook, akimaanisha ukimya wa Marekani.

” Sawa Urusi imewekewa kikwazo jana, lakini hii haitafanya iwe mwisho wa uvamizi dhidi yetu,” amesema.

Akianza mazungumzo yake kwa njia hiyo ya video, Rais huyo ameanza kwa kusema ” Ni siku ya pili tukiwa tena katika vita nzito”.

Pia amesema si kweli kwamba Urusi inashambulia maeneo ya kijeshi tu, bali ukweli ni kwamba ‘haichagui pa kupiga’.

The post Ukraine: Hakuna msaada kutoka kwa washirika wetu appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post