TAASISI YA SARATANI YA OCEAN ROAD KUSIMIKA MASHINE YA KISASA YA UCHUNGUZI WA SARATANI |Shamteeblog.


Na WAF-DSM

Taasisi ya saratani ya Ocean Road inatarajia kusimika mashine ya kisasa ya kufanya uchunguzi saratani mwili inayojulikana kama Positron Emission Tomography – Computerized Tomography scan (PET/CT-Scan) katika mradi wenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 18 ulioanza kutekelezwa Hospitalini hapo.

Akiongelea mradi huo mbele ya Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii, iliyotembelea mapema leo Hospitalini hapo ili kuona utekelezwaji wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Julius Mwaisalage amesema mradi huo ukikamilika utaboresha huduma za saratani nchini kuwa za kiwango cha kimataifa hasa katika uchunguzi wa saratani.

Dkt. Mwaisalage amesema mashine hiyo ni ya kisasa katika uchunguzi wa saratani duniani na itasaidia kugundua saratani mapema Zaidi kwani ina uwezo wa kuonna chembechembe za saratani hata kabla uvimbe haujatokea na pia itakua na kiwanda cha kuzalisha mionzi tiba na kuuza kwenye Hospitali nyingine.

“Machine hii itasaidia kuangalia matokeo ya tiba ili kuona kama saratani imepona, kutokana na ubora wake katika uchunguzi itasaidia kupunguza rufaa za nje na hivyo kuokoa fedha za Serikali takribani Shilingi Bilioni 5 kwa mwaka ambazo utumika kugharamia wagonjwa wa nje ya nchi hasa India”. Amesema Dkt. Mwaisalage.

Dkt. Mwaisalage amewaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa ujenzi wa jengo la kusimika mashine hiyo hadi sasa umefikia asilimia 74 huku ufungaji wa mashine ukitarajiwa kuanza mwezi Aprili na kukamilika Juni 2022 huku majaribio na kukabidhi ikiwa ni Julai mwaka huu.

Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Stansilaus Nyogo ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha shilingi Bilioni 14.5 kwa ajili ya mradi huo ambao utakua unatoa huduma za kisasa Zaidi za uchunguzi wa saratani ambapo huduma hiyo haipatikani katika ukanda wa nchi za kusini mwa jangwa la sahara isipokuwa Kenya na Afrika Kusini pekee.

“Napenda niipongeze Serikali kwani tiba hii ni ya kimataifa ambayo itakwenda kuitangaza nchi yetu kwani itakua na huduma bora za uchunguzi wa saratani na ufuatiliaji wa tiba kuona kama saratani imepona au bado”. Amesema Nyogo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema








 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post