UTEKELEZAJI WA KANUNI ZA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA UMEKUWA WENYE MAFANIKIO MAKUBWA-BoT. |Shamteeblog.


Benki kuu ya Tanzania (BoT) imesema utekelezaji wa kanuni za Huduma ndogo za Fedha,umekuwa na mafanikio makubwa kati ya Watoa huduma na Wateja

Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha BoT, Bw. Deogratias Mnyamani amesema hivi sasa BoT inapata takwimu sahihi kutoka kwenye Sekta hiyo ambapo hapo awali kabla ya Sheria hiyo haikuwa rahisi, lakini pia sheria imesaidia kuondoa soko holela na hivyo kumlinda mlaji, kuongezeka kwa fursa za mikopo na uwekezaji na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi..

Bw. Mnyamani aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha kwenye Semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi, Biashara na Fedha inayofanyika ukumbi wa BoT, jijini Mbeya.

"kumekuwepo na ongezeko la wigo wa biashara rasmi ambapo maombi zaidi ya 1,195 yameshawasilishwa na Wakopeshaji zaidi ya 720 wameshapewa leseni na BOT; pia Maombi zaidi ya 1,125 yameshawasilishwa SACCOS zaidi ya 610 zimeshapewa leseni na TCDC sambamba na Vikundi takriban 25,000 vimekwishasajiliwa na Halmashauri nchini kote'',alisema Mnyamani.

Alisema Watanzania wengi wamejumuishwa kwenye Huduma za Fedha na kumekuwepo na ushindani katika taasisi ikiwa ni pamoja na ongezeko la uwazi.

''Ili kuhakikisha kunakuwepo kwa uwazi katika sekta, BoT iko mbioni kuandaa jukwaa la kielektroniki la kupata taarifa za huduma, njia ambayo itawasaidia walaji kuwa na wigo mpana wa kuchagua wapi akapate huduma'',alifafanua Mnyamani.

Alisema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha Novemba 23, 2018 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2017, ambayo pamoja na mambo mengine ilibainisha umuhimu wa kuwepo kwa Sheria na Kanuni ili kudhibiti mapungufu katika sekta husika.

“Madhumuni makubwa ya Sheria hiyo ni kutoa mamlaka ya Kusajili, Kutunga Kanuni na Kusimamia biashara ya huduma ndogo za fedha na masuala mengine.” Alisema.



Afisa Mkuu Mwandamizi, Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Deogratias Mnyamani akiwasilisha Mada kuhusu kanuni za Huduma ndogo za Fedha katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha jijini Mbeya.


Mmoja wa washiriki wa Semina akisoma muongozo mfupi kwa Washiriki wenzake kabla ya kuanza kwa siku ya pili ya Semina hiyo.
Mmoja wa Waanishi wakongwe ,Lauden Mwambo akifuatilia kwa makini mada zilipokuwa zikiwasilishwa ukumbini humo


Kaimu Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Vicky Msina akitoa maelekezo mafupi kwa Washiriki wa Semina hiyo.






Pichani kushoto ni Afisa Uhusiano Mkuu wa Benki kuu ya Tanzania Lwaga Mwambande akihakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika siku ya pili ya semina hiyo inayoendelea ndani ya tawi la BoT,jijini Mbeya




Waandishi wa habari za Uchumi ,biashara na fedha wakisikiliza yaliyokuuwa yakijiri ukumbini humo kwenye Semina ya siku Tano inayofanyika katika tawi la BoT Mkoani Mbeya.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post