Serikali imetangaza kuondoa tozo ya Sh. 100 katika mafuta.
Hii ina lengo la kudhibiti kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine.
Taarifa iliyotolewa leo na Wizara Ya Nishati imesema Tozo iliyotolewa ni ya Sh 100 kwa kila lita katika Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa kwa miezi mitatu.
Wizara ya Nishati imetangaza maamuzi hayo ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza Machi 2, 2022 huku tathimini ya mwenendo wa soko la dunia ikiendelea.
Maamuzi hayo yataipunguzia Serikali mapato ya Sh bilioni 30 kwa mwezi.
Bei mpya zitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
The post Serikali yaondoa tozo ya Sh100 katika mafuta appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment