Abiria zaidi ya 50 waliokua wakisafiri kwa basi la Kampuni ya Skyline linalofanya safari zake za Dar es Salaam na Katesh Wilayani Hanang mkoani Manyara wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuteketea kwa moto likiwa njiani latika eneo Mtumbatu Wilayani Kilosa mpakani kabisa na Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema waliona moto mkubwa chini ya gari hilo na kuanza kupiga kelele kwa dereva ambapo abiria waliokua ndani ya gari waliposikia kelele hizo ndipo nao walipopaza sauti mpaka Dereva wa basi aliposimamisha.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga aliyefika katika eneo la ajali akifuatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Kilosa Shaaban Mdoe pamoja na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama na kuzungumza na abiria hao alisema anachoshukuru ni kwamba hakuna madhara makubwa yaliyotokana na ajali hiyo ikiwemo majeruhi wala vifo.
DC Mwanga aliwatoa hofu abiria hao kwani ulinzi na usalama wao pamoja na Mali zilizosalia utakuwa mkubwa wakati wote hadi pale usafiri wa kuwachukua na kuwafikisha mwisho wa safari yao.
from Author
Post a Comment