Kipanya: Nilitumia miaka 2 kubuni gari hili |Shamteeblog.

Mtangazaji Ali Masoud, maarufu kama ‘ Kipanya’ amesema ametumia miaka miwili kuunda gari lake la kwanza linalotumia umeme.

Kipanya, ambaye pia ni mchora katuni na mjasiriamali, amesema wakati anaanza ubunifu huo, alipitia wakati mgumu , huku akitumia rasilimali zake binafsi kuhakikisha wazo lake linafanikiwa.

” Waafrika tunaweza kufanya mambo makubwa, muhimu kujiamini na kuzifanya ndoto zetu kuwa kweli,”

” Tulishazoea kuona wazungu na watu wengine wa mataifa yaliyoendelea wanafanya mambo haya, lakini Waafrika tunaweza pia ,” amesema.

Amesema anahitaji mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 3 ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na mwisho wa siku kutoa ajira kwa vijana kupitia magari hayo yasiyotumia mafuta.

” Tutayauza kwa bei nafuu ili watu wayatumie kwa shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo katika nchi yetu,”

Amesema karakana yake imetengeneza magari matatu, moja limekamilika tayari na mengine mawili yapo mbioni.

Amesema magari hayo ni ya umeme na kila gari lina sehemu mbili za kuchaji (port).

” Unaweza kulichaji hili gari kwa masaa sita na baada ya hapo unaweza kutembea umbali wa kilometa 60,”

” Hivyo ni gari rafiki kwa mazingira kwa sababu halitumii umeme na likitembea halipi kelele,” amesema.

Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo mabalozi, wafanyabishara na viongozi wa serikali.

The post Kipanya: Nilitumia miaka 2 kubuni gari hili first appeared on KITENGE BLOG.

The post Kipanya: Nilitumia miaka 2 kubuni gari hili appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post