Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hata kama wataifunga Manchester City Jumapili bado watakuwa na safari ngumu ya kuusaka ubingwa wa EPL msimu huu.
Mechi ya Jumapili inachukuliwa kama ndio itakayoamua hatma ya ubingwa kwa timu hizo.
“Kumfunga Manchester City ni ngumu, hii ni kutokana na aina ya mpinzani tutakayekutana naye,”
” Lakini hata kama tutashinda, bado kutakuwa na mechi nyingine ngumu kupelekea mwishoni mwa msimu wa ligi,” amesema.
Kiungo wa Man City Kevin de Bruyne amesema ni muhimu kushinda mechi muhimu ili kutwaa taji hilo.
” Nikiwa kama Mchezaji, nina shauku ya kushinda mechi kubwa na kutwaa ubingwa,” amesema.
Manchester City , chini ya kocha Pep Guardiola ndio wanaongoza ligi kwa alama 73 na Liverpool ni wa pili kwa tofauti ya pointi moja.
The post Klopp: Ubingwa bado hata tukimfunga Man City first appeared on KITENGE BLOG.
The post Klopp: Ubingwa bado hata tukimfunga Man City appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment