Mayweather tena ulingoni |Shamteeblog.

Baada ya kutangaza kustaafu, bondia mstaafu Floyd Mayweather anatarajiwa kurejea tena ulingoni kwa kupigana na Don Moore katika pambano la raundi nane la maonesho ambalo litafanyika Mei 14, 2022, Dubai.

Bondia huyo mwenye miaka 45, pia alipigana pia katika pambano la maonesho kama hilo mwezi June dhidi ya Youtuber Logan Paul.

Mayweather atapigana na mpinzani huyo ambaye alishinda mapambano ya kulipwa 18 kati ya 19 aliyocheza alipokuwa akipigana.

Mara ya mwisho kwa Moore kupanda ulingoni ilikuwa mwaka 2018 wakati Mayweather alistaafu mwaka 2017, pambano lake la mwisho ikiwa ni dhidi ya Conor McGregor, akiweka rekodi ya kucheza mapambano 50 bila kufungwa.

The post Mayweather tena ulingoni first appeared on KITENGE BLOG.

The post Mayweather tena ulingoni appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post