Mwinyi: Tutaboresha maslahi sekta ya afya |Shamteeblog.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa ahadi ya Serikali katika kuimarisha maslahi ya madaktari, wahudumu na wafanyakazi wa kada ya Afya nchini kuwa ipo pale pale na itatekelezwa mapema iwezekanavyo.

Alhaj Dk. Mwinyi amesema hayo katika ufunguzi wa kongamano la Pili la Madaktari na wahudumu wa Afya, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi, Jijini Zanzibar.

Amesema kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na madaktari, wahudumu na wafanyakazi wa kada ya afya, serikali imeweka mazingatio maalum katika kuimarisha stahiki zao, ili kuimarisha utendaji wa kazi.

Alisema baada ya kupitia upya maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya Afya Zanzibar imebainika kuwa hayaendani na ‘scheme of service’ na kubainisha miongoni mwa kasoro iliopo ni ile ya wafanyakazi wa muda mrefu kupata maslahi duni, hivyo akabainisha hatua ya serikali ya kutoa maslahi kuambatana na ‘scheme of service’.

Alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka kipaumbele katika kuimarisha sekta ya afya, ikianzia na uimarishaji wa miundombinu kwa kuhakikisha kila wilaya inakuwa na hospitali ya kisasa ili kuwaondolea usumbufu wananachi kufuata matibabu nje za wilaya zao wanazoishi.

The post Mwinyi: Tutaboresha maslahi sekta ya afya first appeared on KITENGE BLOG.

The post Mwinyi: Tutaboresha maslahi sekta ya afya appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post