Kocha wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amesema hajutii kuifundisha timu hiyo, bali matokeo ndio hayamfurahishi.
United imeshinda michezo mitatu katika mechi zao 12 zilizopita katika michuano mbalimbali na ipo nafasi ya 7 katika msimamo.
Rangnick alijiunga na United mwezi Novemba akichukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer na ameshinda mechi 9 katika mechi 22.
“Sijutii chochote,” amesema Rangnick kuelekea mchezo wake wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Norwich City.
“Ukiwa kama kocha, unapenda upate matokeo, lakini wakati mwingine haiwezi kuwa unavyotaka,” amesema.
“Katika miezi kadhaa iliyopita, tulionesha tunaweza kuongeza kiwango chetu, lakini mambo yakawa tofauti,” ameongeza.
Rangnick atamaliza majukumu yake mpaka mwisho wa msimu na kupewa kazi ya ushauri klabuni hapo kwa miaka miwili.
Tayari kocha wa Ajax Erik ten Hag amehusishwa kuhamia klabuni hapo.
The post Rangnick: Sijutii kuifundisha United first appeared on KITENGE BLOG.
The post Rangnick: Sijutii kuifundisha United appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment