Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala D. Harris katika Ikulu ya Washington DC Nchini Marekani.
Katika mazungumzo hayo, Rais Samia aliongelea nyanja mbalimbali za maendeleo, ushirikiano na kutoa wito kwa Marekani kuendelea kuwekeza hapa nchini.
Pamoja na mambo mengine, Rais Samia ameupongeza uongozi wa Rais wa Marekani Joe Biden kwa kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo.
Alimwambia mwenyeji wake kuwa Tanzania ilikuwa inafuatilia kwa karibu uchaguzi huo na kuvutiwa Marekani kuwa na Makamu wa Rais mwanamke.
Pia ameishukuru Marekani kwa misaada yake ya maendeleo kwa Tanzania na ushirikiano mzuri uliopo baina ya mataifa mawili.
Katika mkutano huo, Rais amesema Tanzania imepiga hatua katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kupambana na Uviko 19 na kukuza demokrasia, umoja wa kitaifa na mshikamano ili kuleta maendeleo katika jamii.
Lakini pia amesema serikali ya Tanzania inashirikiana vema na sekta binafsi na mashirika ya kitaifa na kimataifa katika kukuza ustawi wa jamii.
Akiwa nchini humo , Rais Samia pia atazindua filamu ya :The Royal Tour’ ambayo ni programu inayolenga kuonesha uwezo wa Tanzania katika sekta za Utalii na Uwekezaji.
The post Rais Samia azungumza na Makamu wa Rais wa Marekani first appeared on KITENGE BLOG.
The post Rais Samia azungumza na Makamu wa Rais wa Marekani appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment