TAASISI YA ELIMU TANZANIA YAZINDUA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA MASOMO YA BIASHARA BAGAMOYO MKOANI PWANI |Shamteeblog.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imezindua mafunzo kazini kwa Walimu wa masomo ya biashara (commerce na book-keeping) yatakayofanyika katika Chuo Cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza katika uzinduzi huo Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Lyabwene Mutahabwa amewaasa walimu watakaopatiwa mafunzo hayo kuyazingatia na kuyafanyia kazi katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji katika maeneo yao ya kazi lengo likiwa ni kuboresha sekta ya elimu nchini.
Amesema ufanisi na utekelezaji utakaotokana na mafunzo hayo utaliwezesha Taifa kufikia lengo la uboreshaji wa elimu unaoendana na matakwa ya kupata nguvu kazi kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.
" Ni matumaini yangu kuwa uboreshaji wa ufundishaji katika taaluma ya ualimu hautaleta tija kwa walimu bali pia utaleta matokeo chanya kwa wanafunzi katika Shule za Sekondari zenye masomo ya michepuo.
Hivyo basi mafunzo haya kwa kiasi kikubwa yataisaidia Wizara ya Elimu kuboresha elimu kwa kutoa wahitimu wenye maarifa, stadi na mwelekeo utakaotokana na ujifunzaji wa masomo hayo yenye tija kubwa katika maisha yao ya kila siku," Amesema Dk Mutahaba.
Amewataka walimu 450 ambao wanahudhuria mafunzo hayo kutumi maarifa na ujuzi watakaoupata katika ufundishaji wao na kuwaambukiza walimu wengine katika maeneo yao ya kazi.
" Ni jambo la kujivunia kwani muda mfupi maarifa na ujuzi huu utakua umesambaa kwa walimu wengi wa shule za sekondari hususani zile zenye mchepuo wa masomo ya biashara," Amesema Dk Mutahaba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk Anneth Komba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia taasisi yao fedha ambazo wamezitumia katika kutoa mafunzo hayo kwa walimu kazini kwa michepuo ya biashara, uchumi na kilimo.
Dk Komba amesema mafunzo hayo yatatolewa katika makundi matatu yatakayohusisha jumla ya walimu 980 kutoka shule za sekondari za serikali na zisizo za serikali ambapo kundi la kwanza ni hili linaloanza leo la walimu 490 wa masomo ya biashara na watahudhuria mafunzo hayo kwa muda wa siku sita.
Kundi la pili litakua la walimu 90 wa masomo ya ufundi watakaopata mafunzo haya katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga kwa muda wa siku sita kuanzia Aprili 20 hadi 25 mwaka huu.
" Kundi la tatu lenyewe litakua na jumla ya walimu 400 wa masomo ya uchumi na kilimo na watahudhuria mafunzo haya katika Chuo cha Ualimu Morogoro kwa muda wa siku sita kuanzia Mei 1 hadi Mei sita mwaka huu," Amesema Dk Komba.
Amesema lengo kuu ni kuwajengea walimu hao uwezo wa kufundisha masomo hayo ya michepuo kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo kuleta tija katika ufundishaji na ujifunzaji na hivyo kuinua kiwango cha ubora wa elimu nchini.
Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Lyabwene Mutahabwa akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Lyabwene Mutahabwa akifafanua jambo kwa Washiriki wa mafunzo kazini [kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce], katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET),Dkt.Aneth Komba akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt. Charles E. Msonde akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) · Dkt. Fika Mwakabungu akiikaribisha Meza kuu kwa kuwatambulisha mbele ya Washiriki wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt Siston Masanja akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Viongozi wa Meza kuu wakiwa wamesimama kwa pamoja wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa ukiimbwa kabla ya uzinduzi wa mafunzo kazini kwa Walimu hao kutoka Tanzania bara na Visiwani.
Mmoja wa walimuwa masomo ya Book keeping na Commerce akiuliza swali ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo
Walimu wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo kwa umakini
Baadhi ya walimu wa Book keeping na Commerce wakiwa katika ufunguzi wa mafunzo kazini kwa Walimu wa Masomo ya Book keeping na Commerce katika Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) leo Aprili 8,2022 wilayani Bagamoyo. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.
By Mpekuzi
Post a Comment