Katika kuonyesha siasa sio uadui, chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema) kinategemewa kukutana na Chama tawala cha Mapinduzi ( CCM) kwa ajili ya kujadili pamoja na mambo mengine, mwelekeo wa kisiasa hapa nchini.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema mkutano huo pia utakukuwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa katika kikao chake na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Dar es Salaam alipokutana naye baada ya kutoka gerezani.
Chadema wamekutana leo katika Mkutano Mkuu Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Pamoja na malengo mengine ya mkutano huo ni kusikiliza rufaa ya wabunge 19 wa Viti Maalum wa chama hicho waliosimamishwa kwa sababu ya kuingia bungeni kinyume na taratibu za chama hicho.
The post Chadema, CCM katika meza moja first appeared on KITENGE BLOG.
The post Chadema, CCM katika meza moja appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment