Simba mdogo mdogo kuisogelea Yanga, yaifunga Kagera Sugar 2-0 |Shamteeblog.

Mabingwa watetezi Simba wamezidi kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao Yanga baada ya kuwafunga Kagera Sugar 2-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Simba imefikisha alama 49 ikiwa ni alama 8 nyuma ya YangaSC inayoongoza Ligi hiyo.

Kabla ya mechi hiyo, Yanga walikuwa mbele kwa pointi 11.

Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Kibu Denis katika dakika ya 12 na John Bocco katika dakika ya 29 yaliipa Simba pointi tatu muhimu.

Dakika 50 Simba ilitaka kupata bao la tatu baada ya Ousmane Sakho kupiga krosi iliyokutana na Kibu Denis ambaye umakini wake kumuangalia kipa wa Kagera Sugar ulikuwa mdogo baada ya kupiga mpira na kuishia mikononi kwa kipa.

Simba waliendelea na kosa kosa ambazo zingeweza kuwapa zaidi ya magoli mawili.

Lakini umakini ukikosekana katika umaliziaji.

Dakika 53 kiungo Ally Idd wa Kagera alipewa kadi ya njano wakati huo huo timu yake ilifanya mabadiliko ya kutoa Hamis Kizza na Ally Idd na nafasi zao waliingia Mbaraka Yusuph na Erick Mwijage.

Dakika 56 kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Mbaraka Yusuph ambaye alikimbia na mpira kwa spidi akipasua katikati ya wachezaji wa Simba.

The post Simba mdogo mdogo kuisogelea Yanga, yaifunga Kagera Sugar 2-0 first appeared on KITENGE BLOG.

The post Simba mdogo mdogo kuisogelea Yanga, yaifunga Kagera Sugar 2-0 appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post