Adaiwa kukutwa na viungo vya binadamu |Shamteeblog.

Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Gwanumpu wilayani Kakonko mkoani Kigoma akidaiwa kukutwa na viungo vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu.

Vitu anavyodaiwa kukutwa navyo ni pamoja na fuvu la kichwa, mfupa wa taya na vinginevyo.

Filemon Makungu, Mkuu wa Polisi wa Kigoma amesema uchunguzi ukikamilika mtu huyo atafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani Kigoma linawashikilia watu watano ambao ni wakazi wa wilaya ya Kasulu kwa tuhuma za kukutwa na lita mia saba za mafuta ya wizi aina ya Diesel wanayodaiwa kuyaiba katika mitambo na magari yanayofanya kazi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Kasulu – Manyovu.

The post Adaiwa kukutwa na viungo vya binadamu appeared first on KITENGE BLOG.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post