Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawachunguza makarani wawili wa Sensa ya Watu na Makazi katika Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega mkoani humo kwa tuhuma za wizi wa vishikwambi vya Sensa.
Makarani hao ni Saphina Francis na Yona Mwalongo .
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Gabriel Zakaria ameviambia vyombo vya habari kuwa makarani hao wanadai kuibiwa vishikwambi hivyo majira ya saa tisa usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu, wakiwa wamelala ndani ya nyumba moja.
“Baada ya kuhojiwa na polisi, makarani hao wanadai walifunga mlango na geti lakini hakuna sehemu yoyote ya nyumba waliyokuwa wamelala imevunjwa,”
Hata hivyo, maelezo hayo yanaonekana hayaridhishi na hivyo ameamua kuagiza polisi kuwahoji na kuwachunguza kwa uzembe uliosababisha upotevu wa mali ya umma.
The post Wachunguzwa kwa upotevu wa ‘vishikwambi’ appeared first on KITENGE BLOG.
By Author
Post a Comment