Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Albert John Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Agosti, Mosi, 2022.
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuasa Mkuu wa Mkoa mteule wa Kagera, Albert John Chalamila kuacha utundu katika majukumu ya uongozi katika nafasi anazoteuliwa na Mamlaka.
Rais Samia ameyasema hayo, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha Viongozi hao aliowateua hivi karibuni, Mhe. Samia amesema RC Chalamila ni mfanyakazi mzuri lakini utundu ndio unamsumbua.
“Natumaini sasa umekuwa na akili imetulia sasa, natumaini utanisaidia kwenye masuala mbalimbali lakini bado nakuangalia kwa karibu sana.”Amesema Mhe. Rais
“Wananchi wakija na Mabango, maana yake Wananchi wanalalamika, Mwananchi akija na Bango ujue analalamika. Mimi nilikataa Mabango ili ninyi Viongozi niliowateua mkafanye kazi vizuri bila Wananchi kulalamika, nataka muende kuwahudumia Wananchi.” Ameeleza Mhe. Rais.
Katika uapisho huo wa Viongozi wateule, Rais Samia amewaapisha Wakuu wa Mikoa tisa kwa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa saba, pia wapo Wakuu wa Taasisi na Mashirika mbalimbali tisa ambao amewateua hivi karibuni.
By Mpekuzi
Post a Comment