RAIS SAMIA AWAPA VIPANDE VYAO ALIYOWAKUMBUKA MAJINA BAADA YA KUWAAPISHA |Shamteeblog.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala kwenye hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2022.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapa vipande vyao wale ambao aliwakumbuka majina yao mara baada ya kuwaapisha.

Akizungumza leo Agosti Mosi 2022, Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya amewaapisha wakuu wa Mikoa tisa aliowachagua huku Makatibu wakuu saba na Viongozi tisa wa Taasisi za serikali wakila kiapo cha Maadili katika Utendaji kazi wao. Amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila atakuwa amekua sasa akili imetulia na akawatumikie wananchi katika Mkoa wake.

Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Elias Thomas waachane na Kombati waende kwenye jamii kuwahudumia wananchi na wakaonje maisha ya Uraiani.

Rais Samia amesema kuwa uteuzi sio Mwisho kwa atakayenda kinyume na utendaji kazi wa Rais atamwondoa na atamchagua mwingine.

Amesema kuwa anahitaji Viongozi wenye Sifa, Uwezo, Uaminifu, watendaji kazi na ambao watamsaidia kuleta maendeleo ya nchi na wananchi.

Amesema Wenye sifa, Uwezo na Uaminifu na imani itawaongoza kufanya kazi pamoja.

"Kama kweli wote tutakwenda kwa nia moja, kuziba mianya tukusanye fedha na hiyo fedha inakusanyika." Amesema Rais Samia

Amesema kuwa Kuitikia Kazi iendelee kuna maana yake, Viongozi walioapishwa leo wataenda kupata mafunzo ya kazi iendelee kwa viwango vyake.

"Kwahiyo nihimize sana ukusanyaji wa mapato, lakini tufanye review kwa vile viwango vya ukusanyaji wa mapato."

Hata hivyo Rais Samia amewaasa viongozi hao kuwasaidia wananchi kwa Moyo safi na kwaakili alizowapa Mungu kwani hawana pengine pa kuhudumia zaidi ya Tanzania , " Na Ukifanya Vizuri Mungu nakunyanyua anakupeleka pazuri na ukifanya vibaya iko tu siku Ubaya wako utaonekana na utaadhirika." Amesema Rais Samia


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post