Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hajamuacha hi hivi Mzee wa Mambango ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albart Chalamila kwa kusema kuwa ambango ni utendaji hafifu wa Kiongozi wa eneo husika huku akisema kuwa ndio mdomo wa wananchi.
Akizungumza leo Agosti Mosi 2022 Ikulu jijini Dar es Salam, mara baada ya amewaapisha wakuu wa Mikoa tisa aliowachagua huku Makatibu wakuu saba na Viongozi tisa wa taasisi za serikali wakila kiapo cha Maadili katika Utendaji kazi wao. Amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akawaambie wananchi wake tena waandike tu mabango.
"Wale wanaokuja na Mabango sasa kawaambieni andikeni tuu, japo 'maneno gani' nyie andikeni tuu njoo nayo kesho."
"Yakija mabango maana yake wananchi wanalalamika na kama wananchi wanalalamika, wewe niliyekuamini kwenye hilo eneo kafanye kazi yako
Practise ni kwamba kiongozi anakuja, Waziri Mkuu anakuja mapema mnasavey, mabango mnayakusanya mnayaweka huko mnawanyima wananchi mdomo wa kusemea kama hutaki mabango nenda kafanye kazi yako, mwananchi akija na bango ule ndio mdomo wake wa kulalamika hana mwingine." Amesema Rais Samia
Amesema kuwa mdomo mwingine wa mwananchi ni Mbunge ambapo inategemea anataka kusema nini bungeni na anataka kuacha nini bungeni.
"Lakini akiona hasemewi mdomo wake ni hilo bango."
Rais Samia amesema kuwa yeye alisema hataki kuona mabango kwa maana kwamba Viongozi waende wakafanye kazi zao.
"Mkifanya kazi zenu mwananchi hata kuja na bango lakini kama kuna bango kwenye eneo lako inamaaana viongozi hamkufanya kazi zenu." Amesema Rais Samia
Amewaomba viongozi hao wakafanye kazi na kuwatumikia wananchi aidha Rais Samia amewapongeza walioteuliwa lakini pongezi hizo zisiwalevye kwa wale waliorudi kwenye nafasi zao na wale waliobadilishwa pia ameendelea kuwasisitiza kwenda kufanya kazi.
Kwa upande wa Viongozi waliokula viapo vya Uadilifu vya kuongoza Mashirika ya Umma Rais Samia amesema Mashirika yaliyo mengi hayafanyi vizuri.
"Tumewapeleka huko kwahiyo kasimamieni mashirika ili yafanye Vizuri."
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Chalamila aliwahi kusema wananchi waende na mabango katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Rais Samia alipokuwa na ziara Mkoani humo.
By Mpekuzi
Post a Comment