Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kushirikiana na taasisi zote zinazohusika kushirikiana na kuhakikisha Usalama wa Mazingira unazingatiwa kwenye ushushaji, utunzaji na upakiaji wa Makaa ya Mawe unazingatiwa.
Katibu Mkuu Migire amesema hayo mara ya kukagua eneo linalotunzwa Makaa ya Mawe katika Bandari ya Mtwara na kubaini changamoto ya vumbi jingi katika utunzaji wa Makaa hayo kabla ya kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari hiyo.
“Kuna mzigo mkubwa sana wa makaa ya mawe hapa lakini bado hatujaweza kudhibiti vumbi la mkaa haya lisitoke nje ya bandari, hivyo TPA shirikianeni na wadau wote muhimu ili kuweka mazingira mazuri kwa mzigo usije kuwa na changamoto zaidi za kimazingira na tukaleta athari kwa wanauhudumia mzigo huu na wananchi nje ya bandari hii’ amesisitiza Katibu Mkuu Migire.
Katibu Mkuu Migire zoezi hilo lisiishie kwenye Makaa ya Mawe litazamwe na kwenye utunzaji wa bidhaa zote ambazo kwa sasa zinasafirishwa kwa wingi kupitia bandari hiyo zitazamwe upya ikiwemo Korosho na Simenti ili kutokusanya mapato na kuacha changamoto nyingine bila kushughulikiwa.
Kwa upande wake Msimamizi wa Usafirishaji wa Makaa ya Mawe kutoka kampuni ya Makaa ya Mawe ya Ruvuma, Abdallah Dadafi amesema kuwa tayari wamechukua hatua mbalimbali za kunusuru athari hizo ikiwemo kununua magari maalum yatakayotumika kupunguza ya vumbi linalotokana na ushushaji, utunzaji na upakiaji wa makaa hayo.
Naye Meneja wa Bandari Mtwara James Ng’wandu amesema kuwa kwa mamlaka hiyo imejiwekea lengo la kusafisha tani elfu sitini ya Makaa ya mawe ambapo mpaka sasa imefanikiwa kusafirisha tani elfu arobaini kwa mwezi ambazo husafirishwa kwa wingi kuelekea nchini Nigeria na Bara la Asia.
Katibu Mkuu Myuko mkoani Mtwara kutembelea na kukagua miradi ya taasisi zilizo chini ya Sekta hiyo.
Gari maalum likimwaga maji kwenye Makaa ya Mawe yaliyohifadhiwa katika Bandari ya Mtwara ili kupunguza vumbi. Zaidi ya Tani elfu ishirini za makaa hayo kusafirishwa kila mwezi kupitia bandari ya Mtwara kuelekea nchi za Nigeria na Bara la Asia.
Katibu Mkuu-Uchukuzi Gabriel Migire (kushoto) akimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Abdallah Malela (kulia) baada ya Katibu Mkuu huyo kumtembela Katibu Tawala huyo ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu-Uchukuzi Gabriel Migire (Kulia) akizungumza na wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara wakati alipotembelea Kiwanja hicho Mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu- Uchukuzi Gabriel Migire (Kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara James Ng’wandu mara baada ya kutembelea Bandari ya Mtwara.
By Mpekuzi
Post a Comment