Mwanamitindo wa Instagram Gena Tew amepata matumaini zaidi katika mapambano yake dhidi ya UKIMWI, baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye macho yake na kuanza kuona tena huku akiwa na imani macho yake yatapona kwa asilimia 100.
Gena alipata Upofu kwenye jicho lake la kushoto ila kwa sasa ameanza kutumia jicho hilo. Gena ameiambia TMZ kuwa alipoteza zaidi ya kilo 30 ila kutokana na dawa anazopewa sasa ameanza tena kuongezeka uzito.
Gena ambaye miezi kadha alitrend mitandaoni baada ya kutangaza anaugua UKIMWI anasema ana matumaini kuwa anaweza kuishi maisha mazuri mradi tu aendelee kutumia dawa zake na kuwaona madaktari, ila pia anataka kuwa balozi na mwanga wa matumaini kwa vijana wengine wanaopambana na UKIMWI.
from Author
Post a Comment