Vodacom yawapika watoto kwenye 'bring your child to work' |Shamteeblog.



Mwakilishi kutoka Project inspire akiwaonyesha watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu ya vodacom Tanzania namna ya kuchanganya kemikali wakati wa mafunzo ya kuhamasiha watoto hao kujifunza sayansi wakiwa na umri mdogo na kujifunza kuhusu kazi wanazozifanya wazazi wao, yaliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam juzi. Picha ya Ericky Boniphace


KAMPUNI ya simu ya mkononi Vodacom,  imewaalika watoto wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kufika katika ofisi hizo ili kujifunza mambo ya Sayansi na Teknolojia na kujua kazi zinazofanywa na wazazi wao wakiwa kazini. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo, Dkt. Isaya  Kasyupa kutoka  Project and Inspire amesema kuwa programu hiyo inayoitwa 'bring your child to work' mlete mtoto wako sehemu ambayo unafanya kazi ni mahususi kwa watoto hao kujifunza na kujua nini wazazi wao wanafanya anapokuwa kazini.

"Vodacom ni Shirika ambalo linajihusisha sana na mambo ya Sayansi na Teknolojia hivyo wameona  ni nia njema pia kuwapa fursa watoto wao siyo tu  kujifunza na kuja kujua wazazi wao wanafanya nini kazini bali pia kujifunza mambo mbalimbi ikiwemo kupata marafiki wapya na kuwajengea uwezo katika masomo yao haswa ya sayansi" .

Amesema watoto Umri mbali mbali kuanzia miaka minne hadi 20 wamepewa mafunzo kutoka na umri wao ma ameongeza kuwa ni vema watoto  wakapata kujifunza teknolojia wakiwa na umri mdogo kwani wataipenda. 

"Sasa hivi tunaelekea karne ya 21 ya mambo ya Sayansi na Teknolojia tunashauri watoto wetu kujifunza Sayansi wakiwa bado wadogo ili Taifa lipate wanasayansi wazuri na Vodacom wapate wahandisi wazuri wenye viwango vinavyohitajika,  ndio maana  watoto hawa leo wanatumia vizuri fursa waliyopata ya kujifunza". Amesema Kasyupa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom, Viviana ...
amesema kuwa  huo ni muendelezo wa kuwaruhusu watoto kujifunza kwenye kampuni hiyo kwa muda wa miaka mitano.

  "Tunataka watoto wetu toka wakiwa wadogo waje waone wazazi wao wanafanya kazi gani mama baba anachelewa kufika nyumbani anafanya kazi gani kule ofisini"

"Tumeshirikiana  na kampuni mbalimbali  ambao wamekuja hapa leo wanawafundisha watoto vitu tofuati vya kufanya hasa katika mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Amesema watoto wanawapa mafunzo yataendana na michezo na watakaa kwenye ofisi hizo kuanzia saa sita mchana hadi 12 jioni.

Amesema kuwa watoto hao watajengewa uwezo wa kujifunza mambo mbalimbali wakiwa nyumbani. 

Naye Faith Martin mmoja wa watoto hao amesema kuwa amefurahi kuona anapata uzoefu wa kazi angali shuleni "tuko  hapa Vodacom tumejifunza mambo mengi, kufanyakazi pamoja na wafanyakazi wa kampuni hii"
" Tumejengewa mazingira ya kuipenda sayansi licha ya watoto wengi hupenda kusoma masomo ya arts (sanaa)."amesema Faith. 

 Amesema kuwa  kufanya kazi ni chachu ya maendeleo ya nchi "Tukiipenda na tukiifanyia kazi inaweza kuleta Maendeleo katika nchi yetu, nimependa sana kwamba Vodacom wameanza kuwaleta watoto na kuwafundisha Sayansi sababu wao ndio wataleta Maendeleo zaidi badae."


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post