Mfanyabiashara Debora Mavura ambaye ni mzalishaji na muuuzaji bidhaa za Dekit Slippers akionesha bidhaa hizo wakati wa maonesho ya wajasiriamali maarufu kama Pop Up yaliyofanyika leo Tabata jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maonesho hayo yaliyofanyika leo Tabata Bima jijini Dar es Salaam Bi. Debora amesema lengo la kukutana na wajasiriamali hao ni kutangaza na kuonesha bidhaa zao katika soko la Tabata pamoja na kubadilishana mawazo ya kukuza zaidi biashara zao.
‘’Soko la Tabata ni kubwa, kuna vitu na watu wengi licha ya kuzoeleka kuwa na vitu negative bado kuna vitu vingi positive ikiwemo hivi tunavyoonesha leo ikiwemo bidhaa mbalimbali kupitia vijana kutoka hapa Tabata na maeneo mengine na tutaendelea kuhamasishana katika kushiriki katika maonesho haya ya pamoja na kujijenga zaidi katika biashara kwa ujumla.’’Amesema.
Bi. Debora ambaye mfanyabiashara na mzalishaji wa bidhaa za Dekit Slippers amesema amekuwa akishiriki mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali na kuzichukua changamoto kama fursa ambazo kwa kukutana na wajasiriamali hao watapeana elimu na mwelekeo wa kuboresha biashara zao.
‘’Nimeshiriki mafunzo mengi na changamoto nilizopata nimezifanyia maboresho na kukutana na wafanyabiashara hawa kwa kuwapa promotion ya kutangaza bidhaa zao katika viwanja hivi bure, chakula na vinywaji huku tukiwa na mwelekeo mmoja tuu wa kujiinua na kukuza biashara zetu.’’ Amesema.
Aidha amesema kuwa ataendelea kuwapa nafasi ya kujitangaza pamoja na kuandaa na kushirikisha vijana na wafanyabiashara katika maonesho hayo ili waweze kujikuza kibiashara na kuwainua vijana wengine.
Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo wameshukuru ushirikishwaji wa maonesho ya namna hiyo ambayo husaidia zaidi katika kujitangaza na kuomba maonesho hayo kuwa endelevu.
Maonesho yakiendelea.
Baadhi ya Wateja wakipata huduma.
By Mpekuzi
Post a Comment