WAKULIMA WA SOYA WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA YA ASILI |Shamteeblog.


****************

Na Mwandishi Wetu-Arusha



Wakulima wa zao la Soya (soyalishe) nchini wameshauriwa kutumia mbolea asilia ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Rai hiyo imetolewa na Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kilimo Endelevu ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Bi. Monica Nakei katika maonesho ya 28 ya Nanenane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea viwanja vya Themi Arusha Agosti 2, 2022.

Bi. Monica amesema kwa sasa anafanya utafiti mbolea asilia itokanayo na vimelea vya bakteria jamii ya rhizobia ambayo inasaidia kuongeza virutubisho vya nitrogeni na fosforasi kwa mimea ya Soya.

" nimefanya utafiti wa mbolea hii kupitia zao la Soya na matokeo ni mazuri ,utafiti utakapokamilika mbolea hii itakuwa tayari kwa matumizi" amesema Bi .Monica

Aidha, ameeleza kuwa, mbolea hiyo ina faida nyingi ikiwemo kuimarisha afya ya udongo na kuweka usawa katika mfumo wa ikilojia ya udongo pamoja na kutunza mazingira kama maji, hewa na udongo.

Bi. Monica ameeleza kuwa, faida nyingine ni pamoja na mazao yatokanayo na mbolea hiyo kutokuwa na kemikali zenye kuleta madhara kwa walaji na gharama yake ni nafuu kwa wakulima.

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu iliyolenga kusaidia jamii na kukuza viwanda kupitia tafiti na bunifu zinazofanywa na wanafunzi wa Taasisi hiyo, ambao wanashiriki katika maonesho ya 28 ya nanenane Kanda ya Kaskazini kwa nia ya kutoa elimu na kuonesha bunifu mbalimbali zinazozalishwa na taasisi hiyo.

Mbali na bunifu ya mbolea asilia , Taasisi hiyo imetoa elimu ya migomba iliyoboreshwa, kiatilifu biologia cha kudhibiti wadudu katika zao la Kabeji, upimaji wa udongo , chakula cha samaki chenye lishe, buheri wa Afya,Nutrano,NUSA,Omega -3DHA,Ngwara,Kweme na vyakula visivyo vya kemikali.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post