Wasanii, Wanamichezo Zaidi ya 300 Kupanda Steji ya Sensabika Leaders Club jijini Dar leo |Shamteeblog.

Na Mwandishi Wetu

Likibatizwa jina la Tamasha Kubwa Kuliko la Kuhamasisha Sensa, Census Biggest Event, hatimaye saa na dakika zinayoyoma za dunia, Afrika na Tanzania kujionea Tamasha kubwa la Sensabika linaloanza alfajiri ya  leo Jumapili ya Agosti 21, 2022 mpaka “liamba” kwa Kiswahili cha kale.

Tamasha hilo kubwa linalohitimisha hamasa ya sensa litawakutanisha “wasanii na wanamichezo zaidi ya 300 kwa wale tu watakaopanda stejini,” anasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, aliyefika Leaders usiku huu kukagua maandalizi.

Ratiba ya Tamasha hilo inaonesha matukio makuu ni kama ifuatavyo:

1. Kuanzia saa 12 alfajiri: Mazoezi ya jogging na magari kutoka pande mbalimbali za Dar es Salaam hasa wengi wakianzia Coco Beach kwenda Leaders;

2. Saa 12:30 asubuhi: Viongozi mbalimbali wa Serikali, sekta binafsi na wadau watakusanyika eneo la Green Park Sports Oysterbay na kuanza “Sensabika Match” kuelekea Leaders

3. Saa 1:30 asubuhi makundi mbalimbali yanakutana viwanja vya leaders kwa ajili ya mazoezi ya aerobics na yoga.

4. Kuanzia Saa 2 asbh mpaka saa 11 jioni: Mashindano mbalimbali ya michezo, mapikipiki, muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali B list ya wakali wa Bongofleva na bendi, maigizo na ngonjera.

5. Saa 12 kamili jioni: Mapambano mawili ya utangulizi kisha anapanda jukwaani bondia Karim Mandonga “Mandonga Mtu Kazi.”

6. Saa Moja kamili Usiku Mpaka Liamba: “A list” ya wasanii wa Bongoflevour na bendi watashambulia jukwaa na hadhira kupokea ujumbe rasmi na mahsusi wa “surprise” wa sensa.

Tayari orodha ya wakali wa Bongofleva kama Marioo, Mboso, Sholo Mwamba, Dulla Makabila, Ruby, Kassim Mganga, Mrisho Mpoto, Saraphina, Baker Flavour, TID na wengine zaidi ya 70 wameshathibitisha kushiriki wakiwemo vijana mahiri wa Taifa Cup na Bongo Star Search.

“Hili tukio ni bure na wananchi wote wanakaribishwa kuanzia mazoezi ya asbh mpak usiku na ni asante ya sekta zetu tatu kwa Mhe Rais Mama Samia Suluhu Hassan na ni asante kwa wadau wetu. Tumejitoa kuwahamasisha wananchi na tunaamini mambo yatakwenda vyema Agosti 23,” anasema Dkt. Kedmon Mapana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Sensabika.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiongea na waandishi wa habari jjini Dodoma Agosti 20, 2022, kuhusu Tamasha la Sensabika ambalo litafanyika leo Agosti 21, 2022 katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam kuwahamasisha Watanzania kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika nchini Agosti 23, 2022.






By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post